VETA WAMETAKIWA KUHAKIKISHA WANAANDAA WANAFUNZI WA HOTELI NA UTALII WENYE VIWANGO VYA KIMATAIFA ILI KUKABILIANA NA USHINDANI WA SOKO ULIOPO

Na Woinde Shizza, Arusha  Baraza la ushauri la chuo cha mafunzo ya hoteli na utalii (VHTTI) limetakiwa kuhakikisha linaandaa wanafunz... thumbnail 1 summary
Na Woinde Shizza, Arusha 
Baraza la ushauri la chuo cha mafunzo ya hoteli na utalii (VHTTI) limetakiwa kuhakikisha linaandaa wanafunzi vyema na wenye viwango vya kimataifa ili kukabiliana na ushindani mkubwa ulioko katika sekta ya hoteli na utalii duniani. 
 Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa wakati akizindua baraza hilo jana ndani ya chuo cha hoteli na utalii cha VHTTI kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha . 
 Alisema kuwa kutokana na changamoto kubwa ya hoteli zetu kuajiri watu kutoka nje ya nchi ikiwemo kenya na hata nchi za bara ya ulaya kwa kile kinachodaiwa vijana wazawa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na sekta ya hoteli na utalii hivyo ni wajibu wao kuakikisha wanafundisha wanafunzi ili waweze kuwa na elimu ya kiwango cha kimataifa . 
 Alibainisha kuwa wanatakiwa wahakikishe wanachuo ambao wanawafundisha wanakuwa na sifa zinazotakiwa huku akiongeza kuwa mafunzo wanayofundishwa yawe bora yanayokidhi maitaji ya ajira .
 Aidha alisema kuwa iwapo watawafundisha wanafunzi hao vyema na kuwapa elimu inayoitajika kuoendana na soko hii itawasaida kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira kwani wanafunzi hawa pindi watakapo maliza elimu yao itakuwa raisi kupata kazi kulingana na elimu walikuwa nayo. 
 ''Pia napenda kuwashauri kuanzisha lunga zote za kimataifa katika chuo chenu ili mwanafunzi anaetoka katika chuo hichi aweze kuwasiliana na mgeni yeyote ambaye atakuja kutoka katika nchi yoyote huko kazini kwake anapoenda kwakweli inachekesha sana kuona mgeni anakuja alafu mwanafunzi anaanza kuongea lugha mfano ya Kingereza kwa kukosea kosea au anaongea Kifaransa  kwa kukose kosea''alisema Munasa 
 Kwa upande wa Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema kuwa wao kama Veta wameamua kuanzisha chuo hichi cha hoteli na utalii ili kuweza kupunguza tatizo la ajira ambalo linaendelea kwa vijana wengi. 
 Aliesema kuwa chuo hichi kitatoa mafunzo ya hoteli na utalii katika ngazi ya cheti na shahada kwa wasimamizi na waangalizi wa hoteli zetu. Naye mkuu wa chuo hicho Flora Hakika alisema kuwa wataji taidi kuwafundisha wanafunzi vyema na wataanza kwa kuaandaa mitaala mipya huku wakiwa wanaangalia zaidi jinsi wenzetu wa nchi za nje wanavyo fanya pia watajitaidi kulenga kupata maitaji ya soko linavyoitaji ili kuweza kuinua zaidi utendaji kazi wa vijana wa kitanzania
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa akiwa anaongea wakati wa uzinduzi  wa baraza la ushauri wa chuo cha mafunzo ya hoteli na utalii cha mamlaka ya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi (VHTTI) Kilichopo Njiro mkoani Arusha
Bw. Mattasia, Mwenyekiti wa Chuo cha hoteli na utalii cha VHTTI akiongea 
wadau mbalimbali wakiwemo wajumbe wa chuo hicho wakiwa wanafatilia uzinduzi huo wa baraza la chuo kwa makini


mkuu wa wilaya ya Arumeru akiwa anamkabidhi nyaraka ya kutendea kazi mmoja wa wajumbe wa baraza la chuo cha VHTTI ambaye ni mwakilishi wa chama cha wamiliki wa makampuni ya utalii(TATO) bw, Peter Lindstrone
Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi (kulia) akifuatiwa na mwenyekiti wa bodi  Bw. Mattasia pamoja na mkuu wa wilaya ya Arumeru  Mhe. Nyerembe Munasa na wakwanza kushoto ni mkuu wa chuo cha VHTTI Flora Hakika wakibadilishana mawazo