KENGE 149 WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE JNIA

  Raia wa Kuwait, Hussain Ahmed Ally Mansour (34), amekamatwa na maofisa usalama na Jeshi la Polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa w... thumbnail 1 summary
 
Raia wa Kuwait, Hussain Ahmed Ally Mansour (34), amekamatwa na maofisa usalama na Jeshi la Polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa tuhuma za kutaka kusafirisha kenge hai 149 wenye thamani ya Sh. milioni 6.33 kwenda nchini Kuwait.
 
Tukio hilo la kusafirisha wanyama hai ni la pili kutokea nchini, la kwanza lilitokea mwaka 2010, baada ya twiga hai wanne waliosafirishwa kwenda nje katika mazingira yenye utata na hivyo kuzua mjadala ndani na nje ya nchi.

 
Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania, Hamis Seleman, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi saa 5:20 usiku akiwa ameficha kenge hao kwenye mifuko midogo 15 ndani ya begi jeusi kwa lengo la kuwasafirisha kwenda Kuwait kupitia Dubai kwa ndege ya Shirika la Emirates.