Chui wa kwenye video ya ‘Pacha Wangu’ ampa Rich Mavoko dili la ubalozi

Yule chui anayeonekana kwenye video ya Rich Mavoko ‘Pacha Wangu’ iliyoshutiwa nchini Afrika Kusini na kuongozwa na Adam Juma amefanya st... thumbnail 1 summary
Yule chui anayeonekana kwenye video ya Rich Mavoko ‘Pacha Wangu’ iliyoshutiwa nchini Afrika Kusini na kuongozwa na Adam Juma amefanya staa huyo kupata dili la Ubalozi wa WWF.
Mavoko chui
Baada ya kupost picha Instagram akisaini mkataba wa ubalozi, Mavoko ameelezea jinsi dili hilo lilivyomfata.
Mavoko mkataba
“WWF ni shirika lisilo la kiserikali linalo jihusisha na Utunzaji wa Mazingira.
Swali: ilikuaje wakanichagua kua Balozi wao?
Jibu: waliangalia video ya #PachaWangu nilivyomtumia Chui walipenda na kuvutiwa na mimi.
2.Walipenda kufanya kazi na kijana ili niweze kuwashawishi vijana wenzangu kutunza Mazingira.”

Chanzo: Bongo5