Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, amesema
Wanyamapori ni moja kati ya rasilimali muhimu inayotoa mchango mkubwa
kiuchumi, kijamii na kimazingira hapa Tanzania na barani Afrika kwa
ujumla.
Amesema kwamba hadi kufikia sasa ni mataifa machache
yaliyobakia yenye wanyamapori wanaopatikana katika mazingira yao ya
asilia kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, uharibifu wa mazingira,
kukinzana kwa shughuli za uhifadhi na kiuchumi (viwanda), mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri
waWizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa na
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keraryo akizungumza na
baadhi ya Watumishi wa Wizara( hawapo pichani) kwenye maadhimisho ya
Siku ya Wanyamapori Duniani yaliyofanyika jana Mpingo House jijini Dar
es Salaam. Mwingine ni Mkurugenzi msaidizi Rasilimali watu, A.R Matagi
Akizungumza na Watumishi wa Wizara pamoja na Waandishi wa Habari
kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani yaliyofanyika jana
kitaifa jijini Dar es Salaam, Mhe Nyalandu amesema kila mmoja lazima
atafakari anafanyaje kuwalinda wanyamapori.
Maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani hufanyika kila tarehe 3 ya mwezi Machi, na nchi mwananchma wa CITES.
Mhe. Nyalandu alisema jamii lazima ilinde na kuhifadhi wanyamapori kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho”.
‘’Tanzania inakabiliana na changamoto kubwa ya ujangili pamoja na
biashara haramu ya meno ya Tembo na na pembe za Faru tushirikiane
Kutokomeza vita dhidi ya ujangili’’ Mhe. Nyalandu alisisitiza
Alisema kuwa Ujangili unahatarisha maisha ya tembo, ujangili na
biashara haramu ya nyara huathiri uchumi wa nchi, ustawi wa siasa,
mifumo ya kiikolojia na usalama wa nchi.
Aliongeza kuwa endapo
wanyamapori hawa watapungua au kupotea Tanzania itaanguka katika utalii
ambao kwa kiasi kikubwa hutegemea Wanyamapori.
Alisema kuwa ili
kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya nyara za tembo na faru
serikali imeamua kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa Idara ya wanyamapori
kwa kuunda Mamlaka ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania “Tanzania Wildlife
Management Authority-TAWA”
Aidha, Mkuju River Uranium Mining
Company (Mantra)” imekabidhi magari mawili aina ya Landcruiser kwa
Wizara ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kusaidia askari wanyamapori
kufanya doria katika mapori nchini