Alikiba na Jacqueline Mengi waungana na serikali na shirika la WildAid katika kampeni dhidi ya Ujangili (Video)

Alikiba na Jacqueline Mengi wameungana na serikali ya Tanzania pamoja na shirika la kimataifa la WildAid katika kampeni dhidi ya ujangili.... thumbnail 1 summary
Alikiba na Jacqueline Mengi wameungana na serikali ya Tanzania pamoja na shirika la kimataifa la WildAid katika kampeni dhidi ya ujangili.
IMG_1409
Mastaa hao pamoja ni miongoni mwa mabalozi wa kampeni hiyo yenye kauli mbiu isemayo ‘Ujangili Unatuumiza Sote.’

Lengo la kampeni hiyo ni kukomesha biashara haramu ya wanyama pori kwa kupungiza mahitaji ya bidhaa zitokanazo na wanyama hao kupitia kampeni za uhamasishaji.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika kwenye hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, mabalozi wa China na Marekani, Alikiba na Jacqueline Mengi na viongozi wa dini.

Wengine waliohudhuria uzinduzi huo ni mwenyekiti mtendaji wa WildAid, Peter Knights na mwenyekiti mtendaji wa African Wildlife Foundation, Dr. Patrick Bergin.

Kampeni hiyo ina lengo la kukuza uelewa kwa wananchi wa Tanzania kuhusu kukithiri kwa uwindaji haramu na kuongeza jitihada za kuwalinda tembo na wanyama wengine wa porini.
Takwimu zinazonesha kuwa Tanzania imepoteza zaidi ya asilimia 60 ya tembo wake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Watu wengine maarufu duniani wanaotumika kwenye kampeni hiyo ni pamoja na Prince William wa Uingereza, Jackie Chan na mchezaji wa zamani wa kikapu wa China Yao Ming.