KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI, SHAABAN MWINJAKA ATEMBELA MAONYESHO YA WIKI YA MAZINGIRA TANGA

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka (mwenye flana ya mistari), akisalimiana na Watumishi wa Wizara ya Uchukuzi n... thumbnail 1 summary
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka (mwenye flana ya mistari), akisalimiana na Watumishi wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake jana katika banda la Wizara ya Uchukuzi katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira Mkoani Tanga. Maonyesho hayo yanafanyika kitaifa mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka akimsikiliza Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi, Yusuph Abdulkadir Muya  wakati akimueleza matumizi ya kifaa cha kupimia mvua jana katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira yanayofanyika Mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka(mwenye flana ya mistari), akiangalia asali katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wakati alipotembelea banda la Wizara hiyo na mabanda mbalimbali jana katika katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira Mkoani Tanga. Maonyesho hayo yanafanyika kitaifa mkoani Tanga.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).