Mabadiliko ya tabianchi yanavyoleta wimbi la magonjwa na wadudu kwenye zao la mahindi

Imefahamika kuwa mimea mingi hasa mazao ya chakula inaandamwa na magonjwa ya aina mbalimbali yanayoleta usumbufu mkubwa na kurudisha ny... thumbnail 1 summary

Imefahamika kuwa mimea mingi hasa mazao ya chakula inaandamwa na magonjwa ya aina mbalimbali yanayoleta usumbufu mkubwa na kurudisha nyuma kilimo pamoja na maendeleo kwa jumla

Waandishi wa habari na bloggers wakizungumza na mmoja wa wakulima wa mahindi, Alfred Mwasi
Changamoto hii unaweza kudhani inewakumba wakulima wa Tanzania pekee, la hasha hili ni tatizo linalowakabili wakulima katika nchi nyingi za kiafrika.

Lakini swala la msingi la kujiuliza ni nini sababu ya kuongezeka kwa magonjwa hayo. “Kadri mvua inapokosekana tunaona magonjwa ya mazao nayo yanaongezeka na kuharibu mazao yetu” anasema Magret Mwasi mmoja wa wakulima kutoka kwenye kijiji cha Kipuzi kwenye Kaunti ya Taita Taveta.

Mama huyu anakiri kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya kupungua kwa mavuno ya zao la mahindi na athari za mabadiliko ya tabianchi, lakini hakuna taarifa za kutosha kuwasaidia wakulima hao kukabiliana na changamoto hizo
Taasisi ya ICIPE inafanya utafiti katika vilima vya Taita nchini Kenya chini ya mradi wa CHIESA ambao unalenga kujua mabadiliko ya tabianchi yanavyoleta athari katika kilimo hasa hasa zao la mahindi.

Mkuu wa mradi huo wa utafiti Paul-Andre Calatayud anasema magonjwa ya zao la mahindi yameongezeka kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuathiri mfumo mzima wa kilimo na utekelezaji wake.

Anasema mabadiliko ya tabianchi yanaweza kusababisha mtawanyiko na wingi wa wadudu waharibifu na hivyo kuharibu mazao ya nafaka mashambani na mavuno yake.

“Utafiti wetu unalenga katika kupata suluhu ya kukabiliana na magonjwa ya mahindi, akiwemo funza (stem borer) ambaye amekuwa ni mharibifu sana katika zao la mahindi na baadae tutatoa majibu ya utafiti wetu ili uweze kutumiwa na wakulima hawa” anasema Paul

Wakulima mahindi katika vijini vinavyozunguka vilima vya Taita wameweka matumaini yao kwenye utafiti huo wakingoja kwa shauku kupata suluhu ya magonjwa na mahindi ambayo yamekuwa mwiba mchungu kwao.

“Tuna matumaini makubwa na utafiti huu, tukiamini kwamba utakuja kutukomboa kutoka kwenye shida hii ya kukosa mazao kila mwaka” anasema Nancy Makio mmoja wa wakulima wa mahindi kutoka kijiji cha Mbengoni Kenya.

Magonjwa yanayoathiri mahindi ni mengi lakini mdudu funza ama bungua amekuwa ni tishio kubwa kwa mahindi sio tu Kenya bali hata hapa nyumbani Tanzania, hivyo kupatikana kwa njia ya kuangamiza mdudu huyo kutaleta tija kwa nchi zote za Afrika Mashariki

Ripoti hii imewezeshwa na Tabianchi kwa kushirikiana CFI chini ya mradi wa Medias21 2015, ikiwa ni juhudi za kutoa elimu ya mabadiliko ya tabianchi kuelekea mkutano wa kimataifa wa mazingira COP21