Mtandao wa haki za
mazingira Barani Afrika (Pan African Climate Justice Allience PACJA), kwa
kushirikiana na Mtandao wa wandishi wa habari za mabadiliko ya tabianchi Zambia
(ZCCN) wameandesha warsha ya siku mbili kwa waandishi wa habari za mazingira
barani Afrika.
Warsha hiyo
inayofanyika mjini Lusaka, Zambia imewashirikisha waandishi wa habari wapatao 30
kutoka nchi mbalimbali za Afrika kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuripoti
habari za mabadiliko ya tabianchi kuelekea kwenye mkutano wa kimataifa wa
mabadiliko ya tabianchi (COP21)
utakaofanyika mjini Paris, Ufaransa Desemba 2015.
Waandishi wa habari za mazingira walioshiriki warsha hiyo kutoka Tanzania ni Dotto Kahindi na Suleiman Shaban
Waandishi
wa habari za mazingira kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwa katika
picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa warsha ya mabadiliko ya tabianchi
unaolenga kuwanoa waandishi hao kuweza kuripoti habari za mkutano wa
mazingira wa kimataifa COP21 utakaofanyika mjini Paris Ufaransa.
Mwakilishi wa UNFCCC nchini Zambia, Richard Lungu akizungumza na waandishi wa habari
Mkufunzi
wa warsha hiyo, Wanjoh Kabukuru kutoka Kenya akifafanua umuhimu wa
waandishi wa habari kuwa wabunifu katika kuandika habari za mabadiliko
ya tabianchi ili ziweze kueleweka kwa jamii
Webstar Whade kutoka Mtandao wa Mabadiliko ya tabianchi na maarifa Afrika (CDKN) akiwa na mwanachama wa PACJA Zambia, Robert Chimambo
Mwandishi
wa habari za sayansi na mzingira Sophie Mbugua (kushoto) kutoka Kenya akiwa na
Mhariri wa jarida la mtandaoni la mazingira la Nigeria
(EnvironewsNigeria) Michael Simire wakati wa warsha hiyo
Waandishi wa habari za mazingira kutoka Madagascar Rivonala na mwandishi Twahinwa Aimabue kutoka Rwanda
#PanAfricanRoadtoParis