Watanzana wametakiwa kutunza na kuthamini mazingira kwa
sababu ni urithi wa thamani kubwa sana kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho
ya wiki ya siku ya mazingira Duniani,
Mheshimiwa Samuel Sita- Waziri wa Uchukuzi ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais
Mhe. Mohammed Gharib Bilal.
Akiongea na Wananchi katika viwanja vya Tangamano vilivyopo
katika jiji la Tanga Mheshimiwa Sita amesisitiza juhudi zaidi katika suala zima
la utunzaji wa mazingira na kuwaomba Wazazi kuelemisha watoto wao umuhimu wa
kuthamini mazingira.
Aidha amewapa hongera Wananchi na Viongozi wa jiji la Tanga
kwa kutilia mkazo usafi wa mazingira na kufanya jiji hilo kuibuka mshindi wa
tatu katika mashindano ya usafi wa mazingira kitaifa.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi ili kufungua sherehe hizo Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Binilith Mahenge aliesma ni jukumu
la kila mmoja kutunza na kuhifadhi
mazingira hivyo basi kila Mwananchi ajitahidi
katika hilo.
Siku ya mazingira duniani hufanyika kila tarehe tano ya mwezi
Juni kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Ndoto bilioni saba, dunia Moja
, tumia Rasilimali kwa uangalifu. Hii
ikimaanisha kutumia vema rasilimali zetu ili kutunza vema mazingira yetu.