Utafiti: Kisiwa cha Zanzibar kiko hatarini kutoweka kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi

Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru, akielezea jamb... thumbnail 1 summary
mazingira 3Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru, akielezea jambokwa wandishi wa habari (hawapo pichani) katika warsha hiyo juu ya mazingira
Na Andrew Chale, Nairobi, Kenya
Wataalamu wa kichunguzi na wanasayansi wa Mazingira, wameelezea kuwa visiwa vilivyopo ndani ya bahari ya Hindi vinatarajiwa kutoweka duniani kutokana na mabadiriko ya tabia nchi inayoikumba dunia kwa sasa ikiwemo upungufu wa kimo cha bahari, ukame na hali ya joto sehemu mbalimbali duniani.
Hayo yameelezwa jijini hapa katika mafunzo juu ya kuripoti habari za mazingira na mabadiriko ya tabia nchi (Climate Change) mafunzo yaliyoanza jana Juni 1, 201a5 ambayo ni maalum kwa wandishi wa habari wanaoandika katika mitandao ya kijamii blog na tovuti kutoka nchi mbalimbali za Afrika, zikiwemo Tanzania, Rwanda, Madagasca, Kenya na Ufaransa ambaoyo ni ya wiki mbili ambao pia ni mkutano wa maandalizi kuelekea katika kongamano la mazingira litakalofanyika jiji la Paris, Ufaransa, Julai na Desemba mwaka huu.
Akielezea hali hiyo, Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru, alibainisha kuwa, visiwa vingi ndani ya bahari ya Hindi ikiwemo Mombasa, Comoro na Madagasca vimo hatarini kutoweka kabisa duniani kutokana na tabia nchi (Climate Change).
“Utafiti mbalimbali umefanyika na kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Dunia itaingia katika matatizo makubwa. Hasa kwa upande wa bahari ardhi iliyo ndani yake kuja kumezwa ikiwemo visiwa vya Zanzibar, Madaga” alieleza Kabukuru ambaye pia ni mchambuzi na mtafiti wa masuala ya mazingira ya ukanda wa bahari anayefanya kazi zake nchini Kenya.
Kwa Tanzania tayari athari mbalimbali zimeanza kujitokeza kutokana na tabia nchi ambapo kwa sasa mmomonyomko wa radhi umeweza kukumba maeneo zaidi ya 148 ambayo yanaingia maji ya chumvi huku wakulima wakishindwa kuendelea na kilimo cha kawaida.
Mkutano huo ulioanza leo Juni Mosi, umeandaliwa na Media Coperation CFI kutoka nchini Ufaransa ulio na lengo la kutafuta njia mbadala juu ya kuripoti habari za mabadiliko ya tabia nchi kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Ufaransa Kenya na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kwa washiriki wa Tanzania,wanawakilishwa na Andrew Chale mtandao wa modewjiblog na Dotto Kahindi mwandishi wa habari wa kujitegemea.
mazingira2Wanahabari wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru (Hayupo pichani) mafunzo hayo yanaendelea jijini Nairobi hadi Juni 11, mwaka huu.
DSC_0466Mwakilishi anayeiwakilisha Tanzania, Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa MODEWJIBLOG.COM, Andrew Chale (kulia) akiwa katika mkutano huo... unaoendelea katika jiji la Nairobi.
wwwAfisa wa CFI, kutoka Paris, Ufaransa, Anne-Sophie Ricco akielezea jambo juu ya mkutano huo kwa wandishi wa habari wa tovuti na blog (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa Safari Club, Jijini Nairobi, Kenya.