Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan ametoa wito wa kutunza mali asili na mazingira kwa sababu ni
urithi kwa vizazi vijavyo.
Aliongea hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Wadau unaohusiana na Azimio la Gaborone jijini Dar es Salaam.
Aliongeza
kuwa idadi ya watu duniani inazidi kuongezeka hivyo basi ni jukumu la
kila mmoja kuacha kukata miti hovyo, kuacha kuchoma misitu na vitu vyote
vinavyosababisha uharibifu wa mazingira kwa sababu upo uhusiano wa
karibu sana kati ya umaskini na uharibifu wa mazingira.
'Uharibifu wa mazingira huongoza kusababisha umaskini' alisema Bi Samia.
Aidha alisisitiza kuwa matokeo yataonekana iwapo maazimio yaliyopendekezwa katika Azimio la Gaborone yatatiliwa maanani.
Mkutano huo wa Wadau wa Azimio la Gaborone umeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Serikali ya Botswana.
Wadau mbalimbali wa mambo ya mazingira kutoka Wizara na Taasisi za Serikali wamehudhuria Mkutano huo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan akifungua Mkutano wa Wadau unaohusiana na Azimio la Gaborone juu
ya utunzaji Mazingira jijini Dar es Salaam.
Mtoa mada katika Mkutano huo Bwana Carlos Manuel Rodriguez akiwasilisha mada yake
Sehemu
ya Wadau wa Mkuatano huo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa
Rais-Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan(hayupo pichani) wakati
akifungua Mkutano huo.
Mgeni
Rasmi Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano, Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wadau waliohudhuria
Mkutano huo.