Mkufunzi
na mtafiti, Daktari John Odindi, kutoka chuo kikuu cha KwaZulu-Natal,
Durban nchini Afrika Kusini (kulia) katika mahojiano maalum na
mwandishi wa Habari mwandamizi wa blog ya modewjiblog.com, Andrew
Chale kwenye mkutano wa wanasayansi juu ya mabadiliko ya tabianchi,
unaoendelea kwenye ukumbi wa Makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa
(Picha na Mpiga picha maalum).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[Paris,
Ufaransa] Watafiti kutoka chuo kikuu cha KwaZulu-Natal, Durban nchini
Afrika Kusini wamewasilisha mada juu ya mabadiliko ya tabianchi
kuhusiana na ongezeko la joto kwenye miji (urban temperature increase)
ya Durban, East London na Port Elizabeth kwenye nchi hiyo.
Mada
iliyowasilishwa na Daktari John Odindi katika mkutano mkubwa wa
wanayasansi juu ya siku za usoni na kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi ‘Our Common Future Under Climate Change’ unaofanyika kwenye
makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Ufaransa. Mkutano huo wa siku nne
(Julai 7-10) unawajumuisha wanasayansi zaidi ya 2500 kutoka pembe zote
duniani.
Akizungumza
katika mahojiano maalum, Dk. Odindi ambaye ni mkufunzi na mtafiti
anasema hali ya ongezeko la joto ni kubwa na kupitia utafiti huo
wanashauri jamii kuchukua hatua dhidi ya kukabiliana nayo.
“Utafiti
wetu tuliowasilisha ni tumeangalia namna ya kukabiliana na mabadiliko
ya tabianchi dhidi ya joto katika miji hii kwani linakuwa kubwa kutokana
na ongezeko la makazi mengi ya watu, viwanda na shughuli za kila siku
za wananchi” alibainisha Dk. John Odindi.
Dk.
John Odindi anashauri uhifadhi na utunzaji wa mazingira ya asili
ikiwemo mimea, chemichemi za maji ya asili na mito kulindwa kwani vitu
hivyo ndivyo vinavyosaidia kupunguza hali ya joto mijini.
Hivyo
ansema kupitia mkutano huu wa Wanasayansi, kuelekea mkutano mkuu wa
21 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiriko ya Nchi (COP21)
utakaofanyika Paris , Desemba mwaka huu, anatumai kwamba mataifa
yatajumuika kutafuta muafaka za kupunguza kiwango cha joto duniani.
Pia
anabainisha kuwa, nchi ya Afrika Kusini imejidhatiti katika
kukabiliana na hali hiyo ya tabianchi katika ongezeko la joto mijini
kwani mkutano wa COP17, ulifanyika katika jiji la Durban, Afrika
Kusini.
Mada
hiyo inaenda sanjari na matakwa ya mataifa mbalimbali juu ya
kukabiliana na kiwango cha hali ya joto na nyuzi mbili (to reduce
temperature level by 2 degrees).
Baadhi
ya wanasayansi hao wakiwa katika mkutano huo unaendelea katika ukumbi
wa mikutano wa makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa.. (Picha kwa
hisani ya Christophe Maitre, INRA).
Chanzo: Moblog