NEMC yawapiga msasa wahariri wa habari za mazingira kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini

Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Uenezi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dr. Vedast Makota (kulia)... thumbnail 1 summary
Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Uenezi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dr. Vedast Makota (kulia), akifungua rasmi warsha ya siku mbili ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, kuhusu jinsi ya kuandaa habari za Mazingira, akifungua kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Mhandisi Bonaventure Baya, iliyofanyika katika ukumbi wa Kibo Palace Hotel Mjini Morogoro. Aliyekaa kushoto ni Mwenyekiti wa mkutano huo aliyechaguliwa Bw. Wallace Maugo ambaye pia ni Mhariiri Mtendaji wa gazeti la The Guardian Limited.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakisikiliza kwa makini hotuba inayotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dr. Vedast Makota (hayupo pichani).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dr. Vedast Makota, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha.