KUWA WA KWANZA UTALII WA NDANI:”TEMBELEA HIFADHI UZAWADIKE”

Baadhi ya wanyama wanopatikana nchini Tanzania kupitia mbuga za hifadhi nchini wakiwa katika moja ya maeneo yao  (picha kwa hisani ya  Ki... thumbnail 1 summary
jaBaadhi ya wanyama wanopatikana nchini Tanzania kupitia mbuga za hifadhi nchini wakiwa katika moja ya maeneo yao  (picha kwa hisani ya Kima safaris. www.kimasafaris.ch).
 Na Andrew Chale,modewjiblog

KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA KWA KUSHIRIKIANA NA WAKALA WA UTALII (TOUR OPERATORS)

Ewe Mtanzania tumia fursa hii kutembelea Hifadhi za Taifa ujipatie zawadi kemkem katika kipindi hiki cha kampeni. Pamoja na kwamba utaburudika, kushangaa na kufurahia kuona vivutio vyetu, pia utapata zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa kila atakayetembelea hifadhi wakati huu wa uhamasishaji. Washirika/wadau wetu wapo katika mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Iringa, Morogoro na Mbeya mjini. Kutakuwa na safari za kila wiki, na/au kwa muda wowote utakaopenda. Wadau wetu wako tayari kukuhudumia kwaGHARAMA AMBAYO MTANZANIA UNAIMUDU KABISA.
Fika katika vituo husika au wasiliana nasi ili ujiandikishe na kulipia kisha uruhusu macho yako kushangaa, akili kutulia na moyo wako kufurahia vivutio vyetu vya asili ndani ya hifadhi za Taifa. Hata ukiwa na usafiri wako binafsi inaruhusiwa kutembelea vivutio vyetu na utazawadika pia.
Kadri unavyotembelea mara nyingi ndivyo unavyojikusanyia fursa ya kupata zawadi ya juu kabisa.
  • Zawadi zitakazotolewa ni DVD za wanyama,Vitabu vya wanyama, Tshirts, Kofia, Tai za TANAPA,  zawadi nono ya kwenda kutalii katika  Hifadhi ya Taifa Serengeti au Gombe kwa muda wa siku TATU na kulala katika hotel yenye hadhi ya Nyota tano. Kwa Hifadhi ya Saanane na Kilimanjaro zawadi itatolewa kwa taasisi itakayopeleka idadi kubwa ya watalii.
  • Kampeni hii na zawadi husika haziwahusu wafanyakazi katika kampuni za kitalii na mahoteli yaliyoko ndani na hifadhi.
Mchanganuo wa Zawadi zitakazotolewa. Katika kipindi hiki cha kampeni kwa yeyote atakayetembelea hifadhi zaidi ya mara moja atapata zawadi  isipokuwa kwa hifadhi za Taifa Saanane na Kilimanjaro (Hizi zina zawadi kwa utaratibu tofauti).
  • Ukitembelea hifadhi ya Taifa yoyote zaidi ya mara moja utajipatia DVD yenye wanyama mbalimbali.
  • Ukitembelea hifadhi ya Taifa yoyote zaidi ya mara mbili utapata DVD ya wanyama na fulana ya TANAPA, Kofia au Tai.
  • Ukitembelea hifadhi ya Taifa yoyote zaidi ya mara tatu utajipatia DVD yenye wanyama mbalimbali, fulana, Kofia, Tai na Kitabu cha wanyama.
  • Ukitembelea hifadhi zaidi ya mara nne utapata zawadi zote hapo juu pamoja na zawadi ya juu kabisa ambapo, utapelekwa kutalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti au Gombe (kuangalia sokwe) na kulala katika hotel yenye hadhi ya nyota tano kwa muda wa siku TATU kwa gharama za TANAPA.
Kwa hifadhi za Kilimanjaro na Saanane: Itazawadiwa taasisi au mtu itakayo peleka wageni wengi zaidi kipindi cha kampeni hii Julai- Disemba, 2015.
  • Saanane-Mtu atakayepeleka watalii wasiopungua 1500 atapewa zawadi ya juu  kabisa
  •  Kilimanjaro -Taasisi itakayopeleka watalii wasiopungua   150 kwa kipindi chote cha kampeni itajipatia zawadi ya juu kabisa.
MUDA WA KAMPENI  Kampeni hii itakuwa ya miezi sita (6). Kuanzia Julai 1 hadi Disemba 31, 2015
VITUO VYA KUJIANDIKISHA NA KULIPIA Vituo vipo mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Iringa, Morogoro na Mbeya Wadau wa utalii wote (tour operators) wanakaribishwa kushiriki.
Muhimu kwa watalii wetu:
  • Kujiandikisha jina na namba ya kitambulisho cha aina moja kila aingiapo hifadhini ili tumtambue kwa ajili ya zawadi.
  • Wenye usafiri binafsi wanaweza tembelea hifadhi bila kupitia vituo vilivyotajwa hapo juu.Wazingatie kujiandikisha katika kitabu maalum kilichopo katika lango la kuingilia hifadhini.
  • Huduma za malazi ya bei nafuu ndani ya hifadhi zinapatikana. Vituo vyetu vilivyotajwa hapo juu vitatoa taarifa zote kwa aina ya utalii wowote unaohitaji ndani ya hifadhi.
  • Sheria na taratibu za hifadhi ziendelee kuzingatiwa
KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NASI KUPITIA: email:   marketing@tanzaniaparks.com Simu:  +255784133217/+255765908073 Facebook:  www.facebook.com/tzparks
ja
1658355_633714670029197_548432396_oSuch a wonderful creatures…. Giraffes in Mikumi Naitional Park.
kafulila
10896341_806804676053528_5127456209430529836_oOne of the clear photo captured at Tarangire National Park Last year. You can imagine how close you can be from Elephant if you visit Parks in Tanzania.Do not let this year end without experience this wonderful moment,Travel with Kima safaris. www.kimasafaris.ch