ForumCC imezindua ripoti yake ya fedha za mabadiliko ya tabianchi
kwenye sekta za kilimo na mifugo baada ya kufanya utafiti kwenye wilaya za Kilosa,
Njombe, Singida na Kongwa.
Akiielezea ripoti hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya
ForumCC, Euster Kibona anasema hakuna pesa zilizotengwa kutoka kwenye bajeti ya
serikali katika sekta hizi zinazolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
“Umefika wakati sasa kwa kuangalia uwezekano wa utafutaji wa
fedha katika kulinda na kuhifadhi mabadiliko ya tabianchi ili kupunguza madhara
yanayotokana na mabadiliko hayo ya hali ya hewa” anasema Kibona
Ripoti hiyo imeonyesha pia kuwa pamoja na fedha za mabadiliko
ya tabianchi kutolewa kwa kiasi kidogo sana lakini bado zimekosa usimamizi mzuri, uwazi wa
matumizi yake na ukosefu wa uwakilishi stahiki kwa wadau na washirika katika
eneo husika.
Mkuu katika kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Shakwaande Natai
(kulia) akizindua ripoti hiyo ya fedha za mabadiliko ya tabianchi kwa
kuipakia (upload) kwenye tovuti ya forumcc, huku akipata maelekezo ya
namna ya kufanya hivyo kutoka kwa Afisa Miradi ForumCC, Fazal Issa.
Mkuu katika kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Shakwaande Natai akiwa na baadhi ya viongozi wa Bodi ya ForumCC, Wizara ya Kilimo na wadau wengine wa mabadiliko ya tabianchi.
Wadau wa mabadiliko ya tabianchi wakifuatilia uzinduzi wa ripoti hiyo