Gesi Asilia kutoka Mtwara yafika jijini Dar es salaam

  Mtaalam kutoka Kampuni ya “CPP” (Mkandarasi wa Mradi wa Gesi Asilia) (Kulia) akitoa maelezo ya usalama kabla ya wakuu wa taasisi za TP... thumbnail 1 summary
 Mtaalam kutoka Kampuni ya “CPP” (Mkandarasi wa Mradi wa Gesi Asilia) (Kulia) akitoa maelezo ya usalama kabla ya wakuu wa taasisi za TPDC na TANESCO kuingia katika kituo cha kupokea gesi asilia Kinyerezi, jijini Dar es Salaam, kituo hicho tayari kimeanza kupokea gesi asilia kutoka kiwanda cha kuchakata gesi  Madimba Mkoani Mtwara.
 Mtaalam kutoka Kampuni ya Mhandisi Mshauri Muelekezi (WorleyParsons), Allen Slowe (kulia) akitoa maelezo ya jinsi ya zoezi zima la kupokea gesi asilia linavyoendelea mbele ya Wakuu wa taasisi za TPDC na TANESCO, Kinyerezi, jijini Dar esa Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio (kulia) akakizungumza na waandishi wa habari kuhusu kufika kwa gesi asilia katika kituo cha kupokelea gesi Kinyerezi, jijini Dar es Salaam ikitokea kiwanda cha kuchakata gesi asilia Madimba, Mkoani Mtwara.
Mitambo ya kupokelea gesi asilia eneo la Kinyerezi, jijini Dar es Salaam ambayo imeshaanza kupokea gesi asilia kutoka kiwanda cha kuchakata gesi asilia Madimba Mkoani Mtwara.

Chanzo: Michuzi