Kuna
hali ambayo unaweza kusikia mwenyewe ndani ya nafsi yako endapo
utajikuta kwenye zahma ya kuvamiwa na simba. hivyo ndivyo ilikuwa kwa
watalii hawa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo simba wenye
njaa kali walivamia gari lao.
Simba
walianza kung'ata matairi na walifanikiwa kutia pancha matairi hayo
huku wakitumia muda mwingi kukwarua vioo ili wafanikishe azma yao ya
kula nyama ya binadamu. lakini kwa bahati nzuri walishindwa.
Muongoza
watalii Emmanuel Bayo kutoka Arusha ambaye alishuhudia tukio hilo
anasema hali ilikuwa mbaya zaidi kwa watalii ndani ya gari.