Ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa
Mabadiliko ya Tabianchi wa Nchi Wanachama COP21 uliokuwa ukifanyika Paris,
Ufaransa, ambao ulimalizika kwa kupitisha mkataba mpya wa mabadiliko ya
tabianchi (Paris Agreement), wadau mbalimbali wamekutana kujadili matokeo ya
mkutano huo.
Mkutano huo wa wadau umeandaliwa na ForumCC kwa kushirikiana
na Rosa Luxemburg Stiftung
(RLS) kwa lengo la kuangalia mazidi na mapungufu ya mkataba huo ambao umeweka
historia mpya ya kuelekea juhudi za kupunguza ongezeko la joto duniani,
kukabiliana na kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Miongoni mwa
vipengele vya mkataba huo vilivyojadiliwa na wadau hao ni pamoja na Kiwango cha
nyuzi joto, Upunguzaji wa gesi Joto, Kukabiliana na mabadiliko ya tabainchi,
Uharibifu na upotevu, Fedha za mabadiliko ya tabianchi, Mfumo wa taasisi na
ushiriki wa serikali, waandishi wa habari pamoja na asasi za kiraia kwenye
kuleta mchango wa makubaliano ya mkataba huo.
Picha ya pamoja ya Wadau hao
Mwakilishi
wa ForumCC, Adam Athony akitoa mrejesho wa kilichojiri kwenye Mkutano
wa Mbadailiko ya Tabianchi COP21 uliofanyika Paris, Ufaransa
Mwakilishi wa Rosa Luxemburg
Stiftung (RLS) Afrika Mashariki, Musa Bulegeya (katikati)
akizungumza jambo wakati wa mkutano huo, kulia kwake ni Meneja Miradi
ForumCC Rebecca Muna, wakati kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya ForumCC
Yunista Kibona.
Mwandishi
wa habari na Mmiliki wa mtandao wa Tabianchi, Dotto Kahindi akitoa
mrejesho wa yale aliyojifunza kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi
COP21, Uliofanyika Paris, Ufaransa.
Washiriki wakifuatilia mkutano huo
Mwakilishi
wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ladslaus Kyaruzi akielezea namna
Tanzania ilivyoshiriki kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP21.
Picha zote na Jonathan Sawaya wa ForumCC