Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Mungano, Bw. January Makamba (kulia) akifafanua jambo wakati alipokutana na Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto) makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii jinini Dar es Salaam. (Pili kushoto) ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Adelhelm Meru, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu,Bw. Selestine Gesimba |
Programu
ya kitaifa ya kupanda na kutunza mazingira inaanza mwezi Januari 2016, hii ni kwa mujibu wa Waziri wa
Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe.
Akizungumza
katika kikao cha pamoja na Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira na Mungano, Bw. January Makamba, Waziri Maghembe alieleza kuwa
Tanzania imetenga maeneo makubwa ya hifadhi ya misitu na mazingira ili
kuhifadhi na kuongeza kuwango cha maji nchini.
Profesa
Maghembe ambaye katika serikali iliyopita alikuwa waziri wa maji,
alieleza umuhimu wa miti na misitu katika kuhifadhi maji na umuhimu wa
maji kwa viumbe hai.
"maeneo makubwa haya ya hifadhi ya misitu na
mazingira yametengwa ili yasaidie kupata hewa nzuri kwa afya yetu, maji,
mvua, kuzuia joto kupanda na kupambana na mabiliko ya tabianchi yanayotishia nchi kugeuka
jangwa.” anasema Maghembe
Anasema
kumekuwa na ukataji mkubwa wa miti na uharibifu wa mazingira nchini na
kueleza kwamba programu hii itakayoanza mwezi huu inalenga kuwa na mazingira bora (ecosystem),
upandaji miti na utunzaji wake.
Waziri
amesema kikao cha mawaziri husika cha kuweka mkakati wa
kutekeleza kampeni hiyo ya upandaji miti na utunzaji mazingira cha siku
mbili kitaanza tarehe 16 January na wataalam wa wizara mbili husika
tayari wameagiza kuandaa kwa pamoja mkakati utakaotumika kutekeleza
programu hiyo.
Mkutano wa pamoja utazingatia masuala yote ya upatikanaji wa rasirimali
zitokanazo na faida ya misitu na mazingira.
Waziri
katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano,Bw. January
Makamba anasema suala la mazingira linagusa shughuli za wizara zote na
taasisi nyingi na sekta binafsi na kueleza kuwa kuna kila sababu ya
vyombo mbali mbali kushirikiana.
Amesema
programu hii ya kitaifa ni ya aina yake nchini na katika utaratibu
huu TAMISEMI itawashirikisha wananchi ili kila mwananchi ajivumie
kupanda miti katika eneo lake.
“Tukitekeleza
programu hii kwa uangalifu na kufanikiwa matunda yake yatavutia watu
wote wa ndani na nje ya nchi kwa faiada ya taifa letu,” anasema Makamba.