Kikongwe avunja rekodi kwa kupanda Mlima Kilimanjaro

Tanzania yamuingiza mwanamke kikongwe kwenye Kitabu cha kumbukumbu za Guinness  baada ya kupanda mlima Kilimanjaro ambao... thumbnail 1 summary
Tanzania yamuingiza mwanamke kikongwe kwenye Kitabu cha kumbukumbu za Guinness  baada ya kupanda mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote Barani Afrika.

Kwa mujibu wa mtandao wa Guinness uliochapisha habari hiyo hivi karibuni ulimwelezea Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Angela Verobeva (86) anakuwa wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro wenye urefu wa (5,895 m; 19340 ft).

Angela Vorobeva amezaliwa Februari 4, 1929.   Amefikia kilele cha Mlima Kilimanjaro,  mnamo Oktoba 29 mwaka 2015. Hata hivyo taarifa zake zimechapishwa mwaka huu 2016 ambapo kwenye taarifa hiyo inaelezea kuwa rekodi yake inaweza kubadilika endapo kikongwe mwingine anaweza kutokea.

Wakati wa upandaji wa mlima huo, Kikongwe huyo alikuwa na kundi la msafara na kupitia lango la Londorossi (2,360 m) mnamo 23 Oktoba 2015 na kufika kelele cha Uhuru Peak (5,895 m) wakati wa mchana siku ya saba (29 Oktoba 2015) ya safari yao nzima.

Kundi hilo lilishuka juu ya kilele hicho cha Uhuru,  30 Oktoba 2015, kupitia lango la Mweka (1,640 m). Mtandao huu Modewji unatoa rai kwa wananchi wa Tanzania kutumia nafasi hii kupanda mlima huo mrefu Barani Afrika kumbukumbu ya kihistoria.

Habari hizi zimeandaliwa na Andrew Chale,modewjiblog.com
kiPicha zinazoonesha akiwa katika harakati za kupanda mlima huo na alipofika kwenye kilele hicho.
mlimaMlima Kilimanjaro.