Tanapa yawakaribisha wasanii kutumia mandhari ya vivutio vya Taifa kwenye kazi zao

Huu ni wakati wa wasanii wa filamu na muziki kuvitumia vivutio vya Taifa katika kazi zao baada ya Meneja wa mawasiliano wa Hifadhi za Taif... thumbnail 1 summary
Huu ni wakati wa wasanii wa filamu na muziki kuvitumia vivutio vya Taifa katika kazi zao baada ya Meneja wa mawasiliano wa Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete, kuwataka wasanii wa filamu nchini kutumia mandhari za asili zilizoko katika hifadhi za Taifa kwa ajili ya kurekodi filamu zao ili kutangaza utalii wa ndani. c9897ec264L
Shelutete alisema hayo katika tamasha la chama cha wasanii wa filamu wa jijini Arusha (TFDAA) katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, akidai kwamba Tanapa itatoa ushirikiano kwa wasanii watakaoonyesha nia ya kurekodi filamu zao katika maeneo ya hifadhi ambayo ni salama na yenye mvuto mkubwa.
“Nchi yetu imejaliwa vivutio vingi hivyo wasanii washirikiane na Tanapa kuutambulisha utalii wetu ili ziweze kuchangia pato la Taifa,” Shelutete aliliambia gazeti la Mtanzania

Naye Rais wa Shirikisho la Silamu nchini (TAFF), Simon Mwakifamba, aliwataka wasanii watumie fursa ya maonyesho ya kimataifa ya filamu yanayojulikana kama Tanzanite International Film Festival yatakayojumuisha wasanii wa filamu kutoka nchi mbalimbali duniani kujitangaza na kutengeneza marafiki wakusaidiana katika sanaa zao.

Chanzo: Bongo5