FORUM CC YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUJADILI MWONGOZO WA KUFANYA USHAWISHI NA UTETEZI KUHUSU MABADILIKO YA TABIANCHI

Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Shakwaanande Natai akifungua kongamano la mabadiliko ya Tabianchi... thumbnail 1 summary
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Shakwaanande Natai akifungua kongamano la mabadiliko ya Tabianchi lenye lengo la kujadili mwongozo wa ushawishi na utetezi katika mipango ya Maendeleo ya Serikali iliyandaliwa na ForumCC na kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka serikarini na sekta binafsi iliyofanyika katika ukumbi wa Sayansi jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona akizungumza jambo wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali kujadili mabadiliko ya Tabia ya nchi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Sayansi jijini Dar es Salaam.
Afisa Miradi kutoka ForumCC, Fazal Issa akitoa mada kuhusu mwongozo wa ushawishi na utetezi wa kuingiza mabadiliko ya Tabianchi katika mipango ya maendeleo ya Serikali pamoja na kupangiwa bajeti kuliko kusubilia majanga yakitokea.
Mratibu wa ForumCC, Rebecca Muna akichangia mada wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira kujadili mabadiliko ya Tabianchi.
 Mchumi kutoka Tume ya Mipango, Jordan Matonya akichangia mada wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za MazingiraTanzania(JET), John Chikomo akichangia mada kuhusu jinsi ya kuripoti habari zinazohusu mabadiliko ya Tabianchi na kuwafunda waandishi wanaoripoti habari za Tabianchi.
Afisa Mifugo kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Theresia Massoy akichangia mada.
Afisa Msaidizi wa Miradi wa ForumCC, Jonathan Sawaya akichangia mada wakati wa kongamano lilowakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira kujadili mabadiliko ya Tabianchi.
Wadau mbalimbali wa Mazingira wakifuatilia mada