MAKAMBA ASIKITISHWA NA UPUNGUFU WA MAJI KATIKA ZIWA RUKWA, ATOA MAAGIZO KWA WAKURUGENZI

Na Lulu Mussa, Sumbawanga Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January Makamba ameendelea na ziara... thumbnail 1 summary
Na Lulu Mussa, Sumbawanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January Makamba ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara yake Waziri Makamba ameshuhudia uharibifumkubwa wa mazingira hususan pembezoni mwa ziwa Rukwa.

Waziri Makamba amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha Nankanga kwamba mwaka 2000 kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka 2016 chanzo hicho kimepungua hadi kufikia mita tatu.

“Tafiti zinaonyesha kuwa kupungua kwa kina hicho pamoja na mambo mengine kunasababishwa na kilimo cha milimani na kandokando ya ziwa, na ulishajiwa mifugo katika Vyanzo vya maji,” Makamba alibainisha.

Katika ziara yake baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri Makamba ameazimia kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa mazingira na kanuni za matumizi ya maeneo hayo zitaandaliwa ilikunusuru Ziwa Rukwa.

Pia, wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa kutenga pesa zitokanazo na tozo mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa alama maalumu ‘beacons’ ili kuainisha eneo tengefu na kuagiza kuwazoezi hili lifanyike haraka.

Aidha, Mhe. Makamba amesisitiza juu ya upandaji wa miti na ameonyesha masikitiko yake kwa Mkoa wa Rukwa kuwa na upungufu wa miti ya asili na ile ya kupanda kwa kiwango kikubwa. “nimetembea zaidi ya kilomita 200 sijaona miti iliyopandwa,” Makamba aliongezea.

Wakazi wa Mkoa wa Rukwa wamefahamishwa na kusisitizwa kuwa kuanzia mwakani itakuwa lazima kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuripoti na miti na kutakiwa kuitunza mpaka pale watakapomaliza shule. Waziri Makamba ameahidi kuleta wataalamu na kutoa orodha ya miche inayostawi katika kila kijiiji ili kurahisisha uoteshaji wa miti.

Katika hatua nyingine, Waziri Makamba amekutana na viongozi mbalimbali wa dini na wazee wa Mkoa wa Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya Amani,na kuahidi kugharamia Mkutano wa kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo nakusisitiza agenda ya mazingira iwepo.

Mkoani Rukwa Waziri Makamba ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo na Mkutano wa Hadhara katika