Forumcc yakutana na wadau kujadili changamoto za upatikanaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona akifungua mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kujadili ma... thumbnail 1 summary
Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona akifungua mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kujadili mabadiliko ya Tabianchi pamoja na changamoto wanazozipata kwenye suala la upatikanaji wa fedha za kuendesha miradi mbalimbali ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Tume ya Sayansi jijini Dar es Salaam. (Picha na Geofrey Adroph)


 Mkurugenzi wa Bodi ya FORUMCC, Dr. Vera Mugittu akizungumzia changamoto za upatikanaji wa fedha nchini Tanzania ili kuendesha miradi mbalimbali ya ukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Abdallah Henku
Jimreeves Naftal kutoka Wizara ya Fedha na Mipango akizungumzia serikali inavyoweza kutoa fedha kwenye masuala ya Tabianchi pamoja na changamoto wanazozipata kama serikali kwenye suala la Mabadiliko ya Tabianchi
Mshauri wa mabadiliko ya Tabianchi, Dr. Lucy SSendi kutoka TAMISEMI akizungumzia kuhusu serikali inavyojikita kwenye utatuzi wa Mabadiliko ya Tabianchi wakati wa kongamano lililoandaliwa na FORUMCC.
Afisa Mwandamizi wa Mazingira kutoka NEMC, Lilian Lukambuzi  akizungumzia miradi wanayoisimamia kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi hapa nchini Tanzania na usambazaji wa fedha kwenye hiyo miradi wakishirikiana na asasi za kiraia zinazohusika na masuala ya Tabianchi
Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Bw. Daniel Marasalama akizungumzia benki ya Dunia inavyofadhili miradi ya Mabadiliko ya Tabianchi kwa nchi zinazoendelea.
 Mkurugenzi Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akiuliza swali kuhusu utoaji wa pesa kwenye miradi inayohusiana na utatuzi wa changamoto mabadiliko ya Tabianchi.
 Baadhi ya wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kutoka sekta binafsi pamoja na serikali kuhusu changamoto wanazozipata katika upatikanaji wa fedha za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi hapa nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akifuatilia mada
 Baadhi ya wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi  wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kuhusu utatuzi wa kuhusu changamoto wanazozipata katika upatikanaji wa fedha za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi hapa nchini.
Baadhi ya wadau wa Tabianchi wakiwa kwenye kongamano lililowakutanisha ili kujadili njia mbalimbali za upatikanaji wa pesa kwa ajili ya miradi inayoendeshwa kwa ajili ya kupunguza mabadiliko ya Tabianchi
Picha ya Pamoja