Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumza katika eneo la uzalishaji mkaa, katika kiwanda cha mkaa poa, mkaa rafiki kwa mazingira mjini Unguja, Kulia ni mmoja wa wafanyakazi katika kiwanda hicho kidogo.
Sample ya Mkaa Poa ulioanikwa juani tayari kupakiwa na kuuuzwa kwa matumizi ya nyumbani
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiangalia mkaa unaoendelea kuwaka moto katika jiko la mkaa ambapo mkaa huo unadaiwa kuwaka kwa masaa matatu.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mkaa Poa cha Mjini Unguja Bw. Bukhet Juma Pamoja na Naibu Waziri Mpina wakiangalia mkaa uliyopo tayari kwamatumizi ya nyumbani.
Wafanyakazi wa kiwanda kidogo chakutengeza mkaa banifu, mkaa rafiki kwa mazingira maarufu kwa jina la Mkaa poa Mjini Unguja wakiwa katika Picha ya Pamoja na Naibu Waziri Mpina Kiwandani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiongea na uongozi wa Mradi wa muungano wa MIVARF pamoja na ujumbe wake katika ziara Mjini Unguja ilohusisha kutembelea Miradi ya Muungano.
Sehemu la eneo la Mto lilitengenezwa na Mradi wa MIVARF katika Mkoa wa Kusini Unguja ili kuweza kusaidia wakaazi wa maeneo ya mabondeni kufanya kilimo hasa katika kipindi cha mvua.
NA Evelyn Mkokoi -
Unguja
Jamii inaweza kuhepukana na mgogoro wa uchafuzi na uharibifu
wa mazingira, utakanao na kukata miti ovyo kwa matumizi ya mkaa, kama itakuwa
na ubunifu wa kutumia teknolojia ya kisasa ya kutengeneza mkaa banifu aina ya
mkaa Poa ambayo ni rafiki wa mazingira,
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshungulikia Muungano
na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameyasema hayo leo Mjini Unguja alipotembelea
kiwanda cha kutengeza mkaa banifu maarufu kama mkaa poa.
Mpina alisema kuwa ukataji ovyo wa miti ya mikoko katika
jamii ya pwani kwa matumizi ya mkaa ni changamoto kubwa ambapo jamii hizi za
pwani zikibuni na kuiga teknolojia ya kutengeneza mkaa kwa kutumia mali ghafi
za taka za mbao yani maranda, taka za maganda ya miwa na taka nyingine laini,
zitakuwa zimejibu tatizo la ukataji wa miti kwa matumizi ya mkaa.
“Matumizi endelevu ya malighafi za taka na mabaki mengine
yanaweza kuwaletea wanachi faida zaidi hasa wakiingia katika biashara hii ya
mkaa poa na kunusuru mazingira, hivyo natoa wito kwa wamiliki wa kiwanda hiki
cha mkaa, waendelee kupanua uzalishaji na kuongeza soko la bidhaa hii hata kwa
upande mwigine wa muungano ili asilimia kubwa ya watanzania ijifunze kutunza
mazingira kwani mkaa huu ni wa bei nafuu, Na wapanue teknolojia hii na kunusuru
mazingira ”Alisisitiza Mpina.
Aidha, Mpina aliishauri serikali kuendela kuunga mkono
jitihada za kampuni hiyo inayotengeza mkaa poa, na watanzania wengine wenye
kufanya biashara za mkaa banifu, ili kuhepusha uharibifu wamazingira, kunusuru
nchi kuwa jangwa na kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia
nchi.
Akiwa Mjini Unguja Naibu Waziri Mpina pia alitembelea miradi
ya muungano iliyopo chini ya TASAF na MIVARF
na kuwapongeza waratibu wa miradi hiyo kwa kuisimamia vizuri na
kujitahidi kwa kiasi Fulani kutatua matatizo na wananchi na kuwaasa kuchukua
taadhari katika utekelezaji wa miradi yao ili kuweza kukabiliana na changamoto
za mabadiliko ya tabianchi hususan katika miradi ya kilimo cha umwagiliaji hasa
katika kipindi hiki ambacho msimu wa mvua umekuwa ukibadilika mara kwa mara.