RC SHINYANGA AWATAHADHALISHA WAHARIBIFU WA MISITU

 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak akizungumza na watalaamu pamoja na wadau wa uhifadhi walioshiriki jana kwenye  kongamano ambalo ... thumbnail 1 summary
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak akizungumza na watalaamu pamoja na wadau wa uhifadhi walioshiriki jana kwenye  kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akijibu hoja zilizotolewa na wadau mbalimbali  wa uhifadhi wa Misitu jana  wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Mdau wa Uhifadhi wa Mazingira, Anna Matinye akichangia hoja  jana kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.
 Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akiwasilisha maada   kwa wadau mbalimbali  wa uhifadhi wa Misitu kwa kuwasomea baadhi ya vipengele kwenye kitabu cha Sera ya Taifa ya Misitu  jana wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Valentine Msusa  akijibu baadhi ya hoja za wadau kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak ( wa tatu kushoto)  akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama wakiangalia baadhi ya miti iliyopandwa katika Shule ya Sekondari ya Kishapu inavyoendelea vizuri kabla ya kuanza kwa kongamano lililofanyika jana  ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa ( watatu kushoto) akiwa pamoja  na Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Zawadi Mbwambo ( wapili kushoto) wakiandika baadhi  hoja zinazowatolewa na  wadau mbalimbali  wa uhifadhi wa Misitu  wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Baadhi ya wadau wa uhifadhi wa Mazingira na Misitu wakifuatilia kongamano lililofanyika jana  ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
Mdau wa Uhifadhi wa Mazingira, Modestus Nyenza  akichangia hoja jana  kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.


Na Lusungu Helela-Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak amewatahadhalisha wananchi kuwa yeyote atakayeharibu misitu kwa kukata au kuingiza mifugo kwenye  misitu atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza jana wilayani Kishapu  wakati wa  kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani humo,  Mkuu wa Mkoa  alipiga marufuku kukata miti bila ruhusa yake au ya Mkuu wa wilaya. 
Telak alisema marufu hiyo imekuja kwa kuchelewa kwa vile hatua iliyofikia  katika Wilaya hiyo  inatisha  hakuna mahindi yanayostawi kutokana  na  kutokuwa na  mvua ya kutosha. 
‘’Mtu yeyote atakayekata miti ajiandae kupelekwa jela  kwa vile kukata miti katika wilaya hii ni sawa na uuaji.’’ alisema Telak
Alifafanua kuwa mtu yeyote atakayetaka kukata miti hata ule uliopo uwanjani pake ni lazima aombe kibali kwa wahusika na atakayekiuka kukata bila kibali ajue jela inamwita.
 Wakati huo huo, Telak  alitoa agizo kwa wakuu wa wilaya wote kuhakikisha wanawakamata wale wote  watakaoingiza mifugo kwenye maeneo yaliyopandwa miti.
Aliongeza kuwa uharibifu wa misitu  unaoendelea kufanyika katika maeneo hayo  unazidi kuathiri hata  mifugo  kutokana na kukosekana kwa malisho kwa vile hakuna mvua inayonyesha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Ezekiel Mwakalukwa  alisema suala la kulinda misitu linahitaji ushirikiano kutoka kwa jamii, wizara pekee haiwezi.
Alisema tatizo la uharibifu wa misitu katika wilaya ya Kishapu limechochea Idara kutengeneza kanzidata itakayosaidia kuzibana Halmashauri kujua imepanda miti mingapi na kati ya hiyo mingapi imepona. 
‘’Tunaanza  mwaka huu kukagua  ili kujua miti hiyo imepandwa wapi na maendeleo yake yakoje’’  alisisitiza  Mwakalukwa.
Amesema hali hiyo itasaidia kuthibiti Halmashauri ambazo zimekuwa zikitaja idadi kubwa ya miti iliyopandwa kila mwaka lakini miti hiyo imekuwa haionekani ikikua na pale unapohitaji kupelekwa ukaone miti hiyo  visingizio lukuki vimekuwa vikiibuka.


Maadhimisho ya wiki ya upandaji miti Kitaifa yanafanyika Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo kauli mbinu yake ni Tanzania ya kijani inawezekana panda miti kwa maendeleo ya viwanda