MTOTO MCHANGA ATUPWA MTO MOROGORO

Wananchi wa mtaa wa Ngoma'A' kata ya Mji Mpya mkoani hapa kwa kuongozwa na mwenyekiti wa Mtaa huo Bi Kidawa Mnyika wa... thumbnail 1 summary




Wananchi wa mtaa wa Ngoma'A' kata ya Mji Mpya mkoani hapa kwa kuongozwa na mwenyekiti wa Mtaa huo Bi Kidawa Mnyika walinunua Mfuko wa rambo na msichana mmoja alijitoa kipande cha khanga kwa lengo la kukistili kimbe hicho kisicho na hatia

Bw Luwanda akiingia kwenye gari la polisi na marehemu huyo wakielekea Mochwari
Majira ya saa 10 jioni mtaa wa Ngoma 'A' kata ya Mji Mpya mkoani hapa Mwili wa mtoto mchanga mwenye jinsia ya kiume ulikutwa ukielea kwenye mto wa Morogoro ukidaiwa kutupwa na mama yake muda mfupi baada ya kujifungua.

Kwa siku za hivi karibuni wimbi la wanawake makatili wa mkoa hapa wamekuwa na tabia ya kutupa watoto muda mfupi baada ya kujifungua bila kuwa na hofu yoyote ya Mungu na serikali kwa ujumla.

Alipotakiwa kuzungumzi tukio hilo mwenyekiti wa mtaa huo Bi Kidawa Mnyika alidai kwamba aliyetupa mtoto huyo hakutoka nje ya mtaa wake na kwamba atafanya uchunguzi wa kina kumbani mwanamke aliyefanya ukatili huo kwenye mtaa wake

" Mimi kama rais wa mtaa huo naamini kabisa aliyefanya ukatili huu anatoka kwenye mtaa wangu hivyo kwa kushirkiana na kamati ya ulinzi shirikishi wamtaa tutafanya kila liwezekanalo kumbaini mwanake aliyefanya unyama huo"alisema mwenyehuo kwa jaziba kubwa

Uchunguzi wa awari uliofanwa na mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba mwanamke aliyefanya ukatili huo alikunywa maji ya uchungu kwa lengo la kujifngua kabla ya miezi tisa kutimia ambapo mtoto huo anaonekana kukaa tumboni kwa miezi 7 au 8