SHIRIKA LA NDEGE LA TANZANIA (ATC) LAZINDUA SAFARI ZAKE ZA DAR ES SALAAM-COMORO.

Na Sophia Yamola Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mwanamvua Ngocho amewaomba Watanzania kutumia fursa ya kufa... thumbnail 1 summary




Na Sophia Yamola
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mwanamvua Ngocho amewaomba Watanzania kutumia fursa ya kufanya biashara katika Visiwa vya Comoro kwa kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa kisiwa hicho wanategemea bidhaa kama vile nguo, vyakula na mahitaji yote muhimu kutoka Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ndege kutua katika uwanja wa ndege wa  kimataifa wa Prince Said Ibrahim Hahaya Mjini Moroni Comoro Ngocho alisema kuwa uzinduzi wa safari za ndege za shirika hilo visiwani humo kutaongeza fursa za kibiashara baina ya nchi hizo mbili.

Aidha aliwashauri wajasiriamali kuchamgamkia fursa hiyo ya kipekee ili kutanua wigo wa biashara, ikizingatiwa kuwa Comoro na Tanzania wanauhusiano mzuri.

Ndege ya ATC itafanya safari zake mara nne kwa wiki katika visiwa hivyo, pia imewahakikishia uhakika wa safari zao na huduma nzuri zinazotolewa bila kusahau ukarimu wa kitanzania.   


Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya ndege ya Tanzania (ATC), Mwanamvua Ngocho akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ndege kutua katika uwanja wa ndege wa  kimataifa wa Prince Said Ibrahim Hahaya Mjini Moroni Comoro