Hali halisi. KAYA 55 Wilayani Magu, mkoa wa Mwanza hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba zao zaidi ya 90 kubomolewa kisha k...
22:59
KAYA 55 Wilayani Magu, mkoa wa Mwanza
hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba zao zaidi ya 90 kubomolewa kisha
kuchomwa moto ikiwa ni sehemu ya kutimiza amri ya serikali za kuwaondoa wananchi wa eneo hilo linalotajwa kuwa ni hifadhi ya taifa.
Tukio hilo la
kinyama linadaiwa kufanyika kuanzia tarehe 1 Agosti hadi Agosti 2 mwaka huu,
ambapo zoezi hilo liliendeshwa chini ya usimamizi wa mkuu mpya wa wilaya hiyo Jaquline
Liana akishirikiana na jeshi la polisi
wilayani humo.
Wakizungumza
na g sengo blog kuhusiana na tukio
hilo, wananchi hao wameilaumu serikali kwa kusema kuwa imeonesha ukatili
wa hali ya juu kwa kuwavunjia nyumba zao, ili hali wakijua kabisa
hawana uwezo hata wa kujenga mabanda kwa mifugo iwe vipi ndani ya muda
wa wiki mbili wawe na mtaji kujenga nyumba za kuishi?.. hakika ni
kitendo
ambacho kinakiuka haki za binadamu na utawala bora.
Wamesema kuwa askari hao walitumia silaha za jadi kuvunja na kuchoma moto nyumba zao.
|
Moja
kati ya waliovunjiwa na kuchomewa nyumba zao Bw. Paulo nkiligila akiwa
na familia yake asijue wapi pa kujisitiri, zaidi ya kuishi chini ya
minyaa
|
Ilielezwa
kuwa kuvunjwa kwa nyumba hizo za vijiji vya Mwabulenga, Misungwi,Bugalu na Salama ni sehemu ya mikakati ya serikali kutaka kugeuza
eneo hilo la Sayaka kuwa hifadhi
ya taifa, ambayo wananchi hao wanadai wamekuwapo zaidi ya miaka 70 tangu enzi za babu zao.
Pichani ni Emmanuel James Salala ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya kijiji.
|
Mmoja
wa wathirika wa tukio hilo, Manhe Mayoka (80) alisema ameishi hapo
akirejea nja ya mwaka 1940 anashangaa leo eneo hilo wanaambiwa wapishe
ni hifadhi ya taifa, mzee huyo amevunjiwa nyumba zake tatu.
|
|
Moja
kati ya familia zilizo athiriwa na bomoa na nyumba zao kuchomwa moto
kutoka kushoto Kija Mahenhe, Rebeca Mahenhe, Maria Mahenhe, Mariam
Manhungwa na mtoto aliyebebwa ni Clement. Familia hii imejisitiri
pembezoni mwa kuta za mwenyekiti wa kitongoji cha Itongo kijiji cha
Bugatu wilayani Magu Bw. Kulwa Ezekiel |
Wananchi
walioathiriwa na kadhia hiyo ni wa vijiji vya Misungwi Kata ya Sukuma na katika
kata ya Ng’aya ni
, Mwabulenga, Salama na
Bugatu wilayani Magu na baadhi ya vijiji vya wilaya ya busega.
|
Hii ndiyo himaya wa mwenyekiti wa kitongoji cha Itongo kijiji cha Bugatu wilayani Magu Bw. Kulwa Ezekiel
|
|
Haya
ndiyo maisha ya wananchi hawa waliovunjiwa nyumba zao kisha kuchomewa,
wamekusanya baadhi ya makuti ya nyumba yao ya zamani na matofali kisha
wakatengeneza kingo na hapo ndipo wanapolala. |
|
Huyu
na familia yake ameamua kuhama la faa lake la kuhifadhia chakula
akijihifadhi pembezoni mwa nyumba ya mwenyekiti kusubiri ujenzi wa
nyumba yake mpya ambao hata hivyo hajajuwa wapi pa kujenga na atajengaje
ile hali hakupata hata fidia kama mtaji wa ujenzi. |
|
Licha
ya kutokujua hatma ya pa kulala vijana hawa kamera yako iliwanasa
wakijisomea kulia ni Ndutu Samson (20) anayesoma kidato cha 4 na
Bukong'one Zacharia (16) anayesoma kidato cha 3, wote katika Shule ya
sekondari Ng'aya wilayani Magu. |
|
Hapa palikuwa bafu.. si waona jiwe la kujisugulia? |
|
Hali tete.... |
|
Wamevunja nyumba zooooote za kizungu lakini hiki kijumba wamekibakiza ... "Au ni Yale mambo ya Vunja Uone?"
by G. Sengo |
|
Ni familia ya watoto watano ya Bi. Sabina Joseph katika makazi mapya. |
|
Naye
huyu akiwa na mwanaye na mumewe hayuko pichani ambao wanatajwa kuwa
walifunga harusi hivi karibuni tu na kupata mtoto huyo kilichofuata
nyumba ikabomolewa na kuchomwa na sasa wanajisitiri pembezoni mwa kuta
za mwenyekiti wao wakisubiri siku isiyofahamika kuishi maisha kama ya
awali yaani ndani ya nyumba. |
|
Mama akihangaika na pichi jiko la nje. |
Batinde Nyaruge mmoja kati ya waliovunjiwa nyumba