Na Walter Mguluchuma, Mpanda
Wakazi wa mji wa mpanda mkoa mpya wa
katavi wameanza kupata huduma ya usafiri wa ndege kuanzai juzi Usafiri huo umeanza kupatikana kufuatia
kampuni ya ndege ya AURIC AIR kuanza safari ya kusafirisha abiria
Ndege hiyo ya kampuni ya AURIC AIR
itakuwa ikifanya safari zake kila siku katika mikoa ya Mwanza, Katavi na Kigoma
Wakazi wa mkoa wa katavi walikuwa
wakilazimika kufuata usafiri wa ndege mjini Sumbawanga mkoani Rukwa pindi
walipokuwa wakihitaji kusafiri
Uwanja wa ndege wa mpanda ambao ni
miongoni mwa viwanja vya ndege vilivyotengenezwa kwa kiwango cha rami toka
ulipokamilika ulikuwa haujawahi kutoa huduma ya kusafirsha abiria
Uanzishwaji wa safari za ndege katika
mkoa wa Katavi utarahisisha watarii na wawekezaji kufika kwa urahisi mkoani
Katavi kwani hapo awali usafiri ulio kuwepo ni wa magari na treni.
Miongoni mwa rasilimali zilizopo mkoani
hapa zilikuwa zinashindwa kufikiwa na wageni kutokana na kutokuwa na uhakika wa
usafiri wa haraka na wa uhakika
Miongoni mwa rasilimali hizo ni Mbuga
ya hifadhi ya Taifa ya Katavi ambayo inasifika kuwa na wanyama wakubwa kuliko
hifadhi zote hapa nchini.
Rasilimali nyingine zilizopo ni madini
ya aina mbalimbali pamoja na kuwa na sehemu ya ardhi ambayo toka kuundwa kwa
ulimwengu haijawahi kutumiwa na binadamu yeyote.