Tunda la Stafeli linatibu saratani

Tunda aina la Stafel TUNDA la stafeli linatibu magonjwa kadhaa, ikiwamo saratani kwa ubora wa karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawai... thumbnail 1 summary


Tunda aina la Stafel
TUNDA la stafeli linatibu magonjwa kadhaa, ikiwamo saratani kwa ubora wa karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawaida yanayopatikana kwenye vituo vya afya, utafiti umebaini.
Utafiti huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dawa cha Purdue nchini Marekani, umeeleza kuwa mbali na kutibu saratani, tunda hilo pia ni tiba ya matatizo ya msongo na mfadhaiko.
“Maajabu ya stafeli ni kwamba lina uwezo wa kuangamiza chembehai zenye saratani pasipo kusababisha madhara katika mwili kama zinavyofanya dawa nyingine za ugonjwa huo au mionzi,” imesema sehemu ya utafiti huo uliochapishwa kwa mara ya kwanza katika Jarida la Kemia na Madawa la nchini Marekani, mwaka 2010.
Taasisi ya  utafiti  wa Saratani ya Nchini Uingereza(NIR) ilifanya  utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mwaka 1976.
Katika utafiti huo ilibainika kuwa majani, mizizi na tunda la stafeli, vina uwezo wa kutibu saratani, lakini matokeo ya utafiti huo hayakutangazwa kwa umma kwa hofu ya kuua viwanda vya dawa za saratani.
Inaelezwa kuwa kirutubisho kilichopo katika stafeli kinatumia  jina la kibiashara la ‘Triamazon’  na kimepigwa marufuku kutumika nchini Uingereza na Marekani  kutokana na uwezo wake mkubwa wa kitiba.
Utafiti mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki nchini Korea na kuchapishwa katika jarida la Bidhaa Asilia  ulibaini kuwa stafeli lina uwezo wa kuponya saratani ya tumbo.


Utafiti wa chuo hicho ulienda mbali na kusema kuwa tunda hilo linaweza kulenga seli za saratani tu, bila kushambulia seli muhimu za mwili kama ambavyo tiba ya mionzi ifanyavyo.

Tunda la Stafeli lina kirutubisho muhimu kiitwacho Annona Muricata, ambacho ndicho chenye uwezo wa kupigana na maradhi ya saratani.
Imeelezwa kuwa stafeli lina uwezo wa kutibu aina 12 za saratani ikiwemo ya matiti, kongosho, mapafu na ya kibofu cha mkojo.
Pamoja na kutibu saratani, kirutubisho hicho kilichopo katika tunda hilo pia huweza kutibu vimelea, shinikizo la damu, msongo wa mawazo, matatizo ya mfumo wa fahamu na sukari.
Utafiti  huo unaonyesha kuwa kirutubisho kimegwacho katika tunda hilo   kinaweza  kwa asilimia kubwa kupambana na saratani bila kumuacha mgonjwa na madhara kama kusikia kichefuchefu, kutapika, kupungua uzito na kunyonyoka nywele.Aidha huweza kuupa mwili kinga na kukupa nguvu  bila madhara yasababishwayo na dawa nyingine.
Tangu mwaka 1976, tunda hilo liliendelea kufanyiwa utafiti  katika maabara binafsi  zaidi ya 20duniani.
 
Stafeli nini?
Stafeli ni tunda la chanikiwiti ambalo linastawi zaidi katika ukanda wa kitropiki.
Mti wa tunda hilo ni mfupi wa wastani, Wabrazili wanauita Graviola na Waingereza wanaliita Soursop. Hapa Tanzani stafeli linajulikana kwa jina jingine la topetope.
Kwa Waingereza, tunda hili ni kubwa lenye uchachu wa kati na utamu mwingi. Ndani yake kuna maganda  yenye weupe kama sufi  na limesheheni juisi.
Mkurugenzi wa Utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Tiba (NIMR) Dk Julius Massaga, alisema taasisi yake haijawahi kufanya  tafiti ya aina yoyote kuhusu tiba ya saratani.
“Tuna kitengo cha masuala ya tiba na mambo mengine lakini hatujawahi kufanyia utafiti tunda la stafeli wala dawa nyingine yoyote ya saratani,” alisema Dk Massaga
Mtaalamu wa masuala ya tiba za vyakula, Boniphas Sosthenes wa kituo cha Tiba cha Neema, jijini Dar es Salaam, alisema anafahamu uwezo huo wa stafeli kutibu saratani, lakini hajathibitisha kitalaamu.
Daktari aliyewahi kumtibu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Dk Keisy Mtambo alisema taarifa za kuwa stafeli linaweza kutibu saratani anazisikia, lakini hana uhakika
“Nasema sina hakika kwa sababu satani ina hatua mbalimbali na kwa watu tofauti,” alisema.
Alisema kwa anavyoifahamu saratani, ni vigumu mno kutibika kwa tunda tu, labda kama tunda hilo limefanyiwa kazi za kitabibu zaidi.
“Kuna saratani kwa watoto, wazee na watu wenye VVU, zina utofauti mkubwa na utafiti huo haujaeleza bayana,” anasema

Una taarifa, picha za usafiri wa anga, mazingira, maliasili na utalii? tutumie kupitia kingkahindi@gmail.com