Katika
hali isiyo ya kawaida chui mmoja amevamia kambi ya watalii kwenye hifadhi ya
Central Kalahari Game reserve huko Botswana na kufanya matukio ya kustaajabisha
likiwemo la kunywa kahawa.
Shuhuda
wa tukio hilo Attie Cilliers alisema chui huyo alifika kambini kwao muda wa
usiku na kunywa maji yaliyokuwa nje na kuondoka zake, lakini ilipofika asubuhi
alirudi tena na kuanza kunusa kila kitu kilichokuwa eneo hilo huku akiweka
ulimi wake kwenye kahawa na kuungua.
Alikaa
kwa muda kusubiri kahawa ipoe na kuendelea kunywa kabla ya kuondoka zake.
Vipande
vya tukio hilo vinaonekana kwenye video ifuatayo