Uharibufu mazingira kikwazo tiba asili

MKURUGENZI wa kliniki ya tiba asili, Dk. Abdallah Mandai, amesema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa tiba asili kutokana na ... thumbnail 1 summary
MKURUGENZI wa kliniki ya tiba asili, Dk. Abdallah Mandai, amesema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa tiba asili kutokana na miti mingi kutoweka.

Kutokana na hali hiyo wameiomba serikali kuwatengea maeneo maalumu kwa ajili ya kuotesha miti ya dawa, ili kurahisisha upatikanaji wake.
Alisema ukosekanaji wa dawa hizo unatokana na changamoto ya uharibifu wa mazingira, mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Dk. Mandai alisema awali walikuwa na tatizo la kutokuwepo kwa chuo kinachofundisha mambo mbalimbali ya tiba asilia, lakini wanashukuru serikali kwa kuwapatia.

Alitoa ushauri sambamba na kuitaka jamii inayotumia tiba asili kuangalia tiba wanazotumia kama zimepimwa au la kwa kuwa kuna waganga wanaotoa dawa bila kuwa na utaalamu wa aina yeyote wala kupimwa maabara.

Chanzo: Tanzania Daima