Fuvu la aliyekuwa chifu wa kabila la Wahehe mkoani Iringa ambaye
alijiuwa kwa kukataa mwili wake kuguswa na wajerumani enzi ya Ukoloni,
kwa sasa limehifadhiwa katika himaya yake kama moja ya kumbukumbu
muhimu za Taifa.
Balozi wa amani nchini Risasi Mwaulanga akiwa na vifaa
vilivyotengenezwa kiasili katika eneo hilo la makumbusho kalenga mkoani
iringa
moja ya kaburi lililopo katika eneo hilo ambalo li la mwanafamilia wa Mkwawa.
Hili ni jengo ambalo ndani ndipo walipohifadhi fuvu hilo na baadhi ya vitu vya asili ya wahehe ambavyo hutumiwa na machifu.
kwa mtu yeyote aliyesoma historia, jina la Chifu Mkwawa halitakuwa geni
masikioni mwake na kwamba kumbuku hiyo ni muhimu kwa vizazi hadi vizazi.
Ikumbukwe kwamba katika chumba hicho kilichohifadhi fuvu halisi la
Mkwawa kwa sasa hutumika kama moja ya makumbusho ya kitaifa na hivyo
kila aliyetaka kufika hapo kwaajili ya kuangalia kwa uhalisia fuvu hilo
ni lazima alipie kiasi cha shilingi 1000 kwa mtu mmoja na kwamba fehda
hizo zinzdaiwa kuwa ni sehemu ya kufanya matumizi ya utunzaji wa mandari
hiyo.
Ama hakika kwa kuangalia kialisia kwa waliofanikiwa kufika katika eneo
hilo mazingira yake yanavutia na kwamba kwa mtazamo wa haraka haraka kwa
nje utadhani nyumba hiyo ni ya kuishi watu.