TAARIFA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA KUHUSU UPOTOSHWAJI WA HALI YA HEWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  WIZARA YA UCHUKUZI        MAMLAKA YA HALI YA HEWA Simu: +255 22 2460706-8 ... thumbnail 1 summary
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 WIZARA YA UCHUKUZI
       MAMLAKA YA HALI YA HEWA

Simu: +255 22 2460706-8
      Telefax: +255 22 2460735, 2460700                                                                                                                                        S.L.P.   3056,
Barua pepe: met@meteo.go.tz                                                                                                                                                    DAR  ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
                                                                                                                                05/05/2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH : UPOTOSHWAJI WA TAHADHARI YA HALI YA HEWA KUHUSIANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini inapenda kukanusha kuhusiana na taarifa ya ujumbe mfupi wa simu na katika mitandao ya kijamii wenye maneno yafuatayo : ‘TMA warning heavy rains of strong easterly winds 100km an hour expected to hit Dar coast from Somalia, Heavy rains 120mm above sea level expected today and tommorrow. People must avoid Sea and areas near to Sea should be alert cautioned. Tanzania Meteorological Agency  www.tma.gov.tz’   
Mamlaka inapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa hiyo siyo ya kweli  na ina  lengo la kupotosha umma na wala haijatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Mamlaka ina kuwakumbusha wananchi wote kuendelea kufuatilia taarifa zetu kupitia vyanzo husika vya Mamlaka vikiwemo utabiri wa kila siku utolewao kupitia radio, televisheni na tovuti ya Mamlaka (www.meteo.go.tz).
Taarifa sahihi za mwenendo wa mvua na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinatolewa  na zinapatikana kupitia njia rasmi za utoaji taarifa maalum za kiofisi (official weather statement).
Hivyo taarifa kuhusiana na mvua zinazoendelea imekuwa ikitolewa katika utabiri wa kila siku kupitia vyombo vya habari, mtandao wa kijamii  wa Mamlaka na tovuti ya Mamlaka.

Tunawatakia shughuli njema katika ujenzi wa Taifa letu.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA