Ndege
ya shirika la AirAsia Indonesia iliyokuwa ikisafiri kutoka Indonesia
kwenda Singapore ikiwa na watu 162 ndani yake imepotea.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200, ilipotea katikati ya safari yake zaidi ya masaa mawili kutoka mji wa Surabaya.
Hali mbaya ya hewa iliripotiwa kutoka kwenye eneo hilo na shughuli za uokozi zimesitishwa hadi Jumatatu asubuhi.
Ndege hiyo ilikuwa na raia 155 wa Indonesia na wengi kutoka Korea Kusini, Ufaransa, Malaysia, Singapore na Uingereza.
Abiria ha ni pamoja na watoto 17.