Misitu ya asili hatarini kutoweka nchini

  MISITU ya asili nchini ipo hatarini kutoweka  kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na binadamu   na kuongezeka kwa joto. ... thumbnail 1 summary
 
MISITU ya asili nchini ipo hatarini kutoweka  kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na binadamu   na kuongezeka kwa joto.

Kutokana na hali hiyo imeelezwa kuwa kuna ya kuibuka kwa kasi magonjwa ya milipuko yanayosababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Balozi wa Mabadiliko ya Tabianchi nchini, Mchungaji Profesa Aidani Msafiri alikuwa akizungumza katika kongamano la vijana na viongozi wa dini mjini Moshi.

Alisema kuwa uoto wa asili nchini umetoweka kwa asilimia 60 kutokana na uharibifu wa mazingira.
Profesa Msafiri alisema jambo hilo limesababisha kukauka  vyanzo vya maji,   kuongezeka   joto kali   na kushuka  kiwango cha uzalishaji wa mazao ya chakula.

“Tanzania kwa sasa imebakia kama jangwa wengine wanaona suala hilo kama mzaha lakini hali ilivyo kwa sasa siyo nzuri.

“Asilimia 40 tu ya miti ya asili ndiyo imebaki,” alisema Profesa Msafiri.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga, alisema hali ya joto kwa mkoa huo imezidi kuwa mbali kuwa na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Alisema  utafiti unaonyesha   baada ya miaka 20 Mkoa wa Kilimanjaro utakuwa kame zaidi kuliko Mkoa wa Dodoma.