Mashirika yatakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa agizo la usafi wa mazingira

Wito umetolewa kwa jamii, Taasisi na wadau mbalimbali kutopunguza kasi katika kutekeleza kwa vitendo agizo la kufanya usa... thumbnail 1 summary
Wito umetolewa kwa jamii, Taasisi na wadau mbalimbali kutopunguza kasi katika kutekeleza kwa vitendo agizo la kufanya usafi wa mazingira, kupanda miti na kulinda vyanzo vya maji alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Desemba  9 mwaka jana.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam ( DAWASA) Bi.Mary Ntikula kufuatia  watumishi wa Mamlaka hiyo na wale wa Shirika la Maji Safi  na Maji Taka Dar esalaam (DAWASCO) kufanya Usafi na kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali hospitalini hapo amesema kuwa wao kama DAWASA wamejiwekea utaratibu wa kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka kila mwisho wa mwezi kuunga mkono agizo la Mhe.Rais la kufanya usafi kila jumamosi mwisho ya kila mwezi.

Amesema katika kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo utaratibu wa kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka yakiwemo ya Hospitali ya Mwananyamala na maeneo mbalimbali ikiwemo vyanzo vya maji pamoja na shughuli za upandaji wa miti kwa lengo la kuhifadhi mazingira.

Ameeleza kuwa Jumamosi ya kwanza ya mwezi huu wao kama DAWASA wameona ni vyema wakaitumia kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali ya Mwanayamala kwa kutambua mchango wa hospitali hiyo katika kuhudumia afya za wagonjwa wanaotoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar essalaam.

Ameongeza kuwa wao kama wafanyakazi wa DAWASA wameungana na wenzao wa DAWASCO kufagia, kufyeka, kusafisha mifereji na kuondoa maji taka katika hospitali hiyo pamoja na kutoa zawadi zinazoendana na usafi zikiwemo maji, mafuta, sabuni za kuogea na kufulia pamoja na mafuta ya kujipaka watoto wadodo na vitu mbalimbali kwa matumizi ya wagonjwa ili kuonyesha upendo wao.

” Leo tumekuja hospitali ya Mwanayamala kufanya usafi na kutoa zawadi, tumezunguka mazingira yote, tumefagia, tumefyeka, tumezoa uchafu na pia kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa zinazohusiana na usafi na nyingine tumewapatia viongozi wa hospitali ili waendelee kudumisha usafi katika hospitali hii” Amesisitiza na kuongeza kwamba wao kama DAWASA wataendelea kusaidia hospitali hiyo katika maeneo mbalimbali.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji wa DAWASCO Mhandisi Shabani Mkwanywe amesema wao kama DAWASCO wameitikia wito wa Mhe.Rais kwa wa kufanya usafi kila jumamosi ya kwanza ya kila mwezi kwa kugawanyika katika maeneo mbalimbali kufanya usafi ikiwemo hospitali ya Muhimbili.

Amesema wao wanafanya kazi na jamii na wataendelea kuwajibika kwa jamii kwa kile wanachokipata na kutoa wito kwa Taasisi na mashirika mengine kuitumia siku hii kufanya usafi ili kuepuka magonjwa ya milipuko.

Aidha, amesema DAWASCO katika kutekeleza majukumu yao wataendelea kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora kwa wananchi ili kuondoa changamoto iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa mkoa wa Dar es salaam na wakazi wa Kibaha na Pwani mkoani Pwani ya uhaba wa maji kufuatia uzalishaji wa maji ya kutosha uliopo sasa.

Naye Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye pia ni Daktari wa watoto, Delila Moshi akizungumza mara baada ya zoezi la usafi wa mazingira na ugawaji  wa misaada katika hospitali hiyo amewashukuru watumishi wa DAWASA na DAWASCO kwa kujitoa na kufanya usafi.

Ameeleza kuwa hospitali hiyo licha ya kupata huduma ya uhakika ya maji safi bado inakabiliwa na changamoto ya uondoaji wa majitaka kwenye mashimo yaliyopo hospitalini hapo kutokana na mfumo wa uliopo kutounganishwa kwenye mfumo mkuu unaopeleka maji taka baharini  jammbo linaloifanya hospitali hiyo kujikuta ikitumia gharama kubwa kuondoa maji hayo.

” Maji taka tunayozalisha kwa siku ni mengi sana, tunawashukuru DAWASA na DAWASCO kujitolea kunyonya maji taka yote katika mashimo sasa tutakaa miezi 6, ninyi wenyewe mtakua mashahidi gharama ya uondoaji wa maji haya ni kubwa tumekuwa na kero ya vyoo kufurika na wakati mwingine kuziba”

Aidha, amesema kuwa hospitali ianaendelea na mradi wa jengo la ghrofa 5 kwa lengo la kupunguza msongamano wa wagonjwa walioko kwenye wodi 11 ambazo zote zimejaa wagonjwa huku akibainisha kwamba hospitali hiyo ina hudumia zaidi ya kniniki 11 pia wagonjwa 1500 hadi 2000 kwa siku.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hospitalini hapo kama walivyofanya DAWASA na DAWASCO.

Nao baadhi ya wagonjwa wa hospitali hiyo waliopata fursa ya kuzumza mara baada ya kukabidhiwa misaada hiyo akiwemo Bi.Stella Mkufya anayeuguza mwanae katika wodi ya watoto hospitalini hapo ameishukuru DAWASA na DAWASCO kwa misaada waliyoitoa.

Amesema kuwa mbali na kupokea misaada ya vitu anafurahishwa na ubora wa huduma zinazotolewa kutoka kwa madaktari wa hospitali hiyo na kuiomba Serikali iendelee kuongeza majengo na vitanda vya wagonjwa katika hospitali hiyo.

” Nawashukuru DAWASA na DAWASCO kwa msaada waliotupatia pia nawashukuru madakatari wa hospitali hii kwa huduma nzuri wanayotupatia, kwa kweli huduma ya hapa ni nzuri sana naiomba Serikali ituongezee vitanda na magodoro” Amesema.
Na.Aron Msigwa-MAELEZO.
imageViongozi wa DAWASA wakishiriki katika zoezi  la usafi. Kutoka kushoto  ni Mary Ntukula, Mkurugenzi wa utawala na kulia ni Eng  Romanus  Mwang’ingo Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi.  Katikati ni Neli Msuya  Meneja mahusiano  ya jamii.
image_2Watumishi wa DAWASA na DAWASCO wakijiandaa kuingia kwenye wodi za wagonjwa kugawa misaada ya vitu mbalimbali.
image_1Baaadhi ya watumishi wa DAWASA wakiendelea na zoezi la usafi katika Hospitali ya Mwananyamala.
image_3 image_4Watumishi wa DAWASA na DAWASCO wakigawa msaada wa vitu mbalimbali kwenye wodi za wagonjwa
image_5Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye pia ni Daktari wa watoto, Delila Moshi akizungumza mara baada ya zoezi la usafi wa mazingira na ugawaji  wa misaada katika hospitali hiyo uliofanywana watumishi wa DAWASA. Picha zote na Aron MSigwa- MAELEZO. .