Kituo cha
ITV kupitia Twitter kimesema mwenyekiti wa jumuiya ya madakatari Dr. Stephen
Ulimboka ametekwa na kupigwa na watu wasiojulikana na anapelekwa katika
hospitali ya mifupa ya Moi.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Jamii Forums Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku
na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana!
Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la
'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa
serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye face to face kwa ajili ya
mazungumzo.
Dokta
huyo aliokotwa akiwa na hali mbaya sana na hawezi kuzungumza.
Tukio
hilo limetokea wakati kumekuwepo na mgomo wa madaktari nchi nzima ambao hata
hivyo wameonekana kusalitiana kwa kutokuwa na msimamo wa pamoja, kwani maeneo
mengine yote huduma zimeendelea kama kawaida, isipokuwa katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Madaktari
hao wametangaza mgomo usio na kikomo kwa lengo la kuishinikiza serikali
kutimiza mahitaji yao, ikiwemo kuboresha mazingira ya kufanyia kazi pamoja na
kuwapandishia mishahara.
Licha ya
mgomo huo kuanza kuleta madhara kwa wagonjwa katika siku ya kwanza juzi, kwa
madaktari kutofanya kazi katika hospitali mbalimbali nchini, jana hali hiyo
ilikuwa tofauti kwani sehemu nyingi huduma ziliendelea kutolewa kama kawaida.
Chanzo: Thisday Magazine