PROFESA LIPUMBA KWENDA KUMJULIA HALI DK LIPUMBA JIONI HII

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi, Profesa Ibrahim Lipumba (kulia), leo saa 10 jioni atakwenda kumtembelea kumjulia hal... thumbnail 1 summary

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi, Profesa Ibrahim Lipumba (kulia), leo saa 10 jioni atakwenda kumtembelea kumjulia hali, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka ambaye amelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jana baada ya kutekwa na kupigwa na watu wasiojulikana.

Askari wakilinda usalama jana wakati Dk. Ulimboka anafikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbi, kupata matibabu.

Mchana huu sakata limetokea kati ya ndugu wa Dk. Ulimboka na waandishi wa habari waliotakiwa na Ulimboka kufanya nao mkutano, kukukataliwa kuingia chama cha ICU, WAKIHOFIA USALAMA WAKE.


Licha ya madaktari kuwakubalia wanahabari kuingia lakini ndugu, akiwemo dadake walikataa katakata. Ndipo Madakatari walipoamiua kuchukua rekoda na kamera za wanahabari na kwenda kumpiga picha wao pamoja na kumrekodi
 
Chanzo: Richard-Mwaikenda blog