Pinda asema litakalo kuwa na liwe
SERIKALI imesema kesho itatoa tamka la mwisho kuhusu
mgomo wa madaktari baada ya Chama cha Madaktari (MAT) kukaidi amri ya Mahakama
Kuu Kitengo cha Kazi ya kusitisha mgomo wao kwa kutangaza kusitisha mgomo huo
kupitia vyombo vya habari.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri
Mkuu Mizengo Pinda wakati akijibu hoja ya mbunge wa CCM Jimbo la
Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi aliyeitaka serikali kutoa tamko juu ya mgomo wa madaktari badala
ya kutumia mahakama kuzuia mgomo huo huku wagonjwa wakindelea kuumia kwa kukosa
huduma.
“Kesho
tutatoa kauli ya mwisho kwa madaktari, litakalo kuwa na liwe” alisema Pinda
Jana Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi imekionya Chama
cha Madaktari Tanzania (MAT) kuhusu utekelezaji wa amri yake ya kusitisha mgomo
wao na kukiagiza rasmi kutangaza kusitisha mgomo huo kupitia vyombo vya habari,
hadi Julai 24, 2012.
Onyo na amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Sekela
Moshi kwa Rais wa MAT akirejea amri aliyoitoa Ijumaa iliyopita akikiagiza chama
hicho na wanachama wake kutoitisha mgomo wala kushiriki katika mgomo huo.
Jaji Sekela alitoa amri hiyo kufuatia maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Serikali ikiomba mahakama isikilize na kutoa uamuzi wa upande mmoja wa kuzuia mgomo huo kwa muda kusubiri usikilizwaji wa pande zote wa maombi hayo.
Amri hiyo ya jana ilikuwa inakazia nyingine ambayo ilitolewa Ijumaa iliyopita, siku ambayo chama hicho kilitangaza kuanza kwa mgomo siku inayofuta.

Hata hivyo amri hiyo haikutekelezwa na chama hicho
na kulikuwepo na madai kwamba viongozi hawakupatiwa nakala ya amri hiyo na hivyo
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) jana ikalazimika kutangaza rasmi
kusitisha baadhi ya huduma zake kutokana na mgomo wa madaktari unaoendelea
nchini na kushika kasi zaidi katika hospitali za rufaa za KCMC, Bugando na
Mbeya