¨
Mazingira yanaipatia nchi mahitaji yote ya msingi kwa ajili ya
kufanikisha masuala ya jamii na uchumi.
¨
Mazingira ndiyo makazi ya viumbe vyote – memea na wanyama ambao ndiyo
urithi usiokuwa na badala yake.
¨
Mazingira ni chombo cha kuweka yale yasiyofaa.
¨
Mazingira ni msingi ambao ndiyo itakuwa jawabu la kupunguza unyonge wa
umaskini.
Kwa hiyo ni dhahiri kwamba
msukumo mkubwa wa uongozi wa mazingira ni kulinda sehemu asili ya kuishi
binadamu na kuoanisha upungufu uliopo kwenye mazingira katika kusaidia kufikia
maamuzi yanayohusu masuala na shughuli za uchumi.
Serikali ya Tanzania
ilitambua hatari ya kupoteza rasilimali hiyo kama vile hewa safi, mabaki ya
mimea na wanyama wa kale, nyangumi, miti ya asili na wanyama/mimea ambayo iko
mbioni kutoweka.
Katika kurekebisha hali
hiyo, serikali imechukua hatua thabiti kwa kutengeneza sera, sheria na mfumo wa
taratibu ambazo zinaendana na masuala ya jamii, uchumi na siasa.
Serikali kwa kushirikiana
na washika dau mbalimbali wameweka mkazo katika kuendeleza kukuza na
kuhamasisha ushirikishwaji wa jumuiya na watu binafsi katika kuimarisha
uhifadhi na uongozi wa mazingira. Pamoja
na hayo kulikuwa na kampeni za kutambua umuhimu wa mazingira, elimu ya
mazingira na kuendeleza ujuzi ambao ulisaidia katika kuhifadhi na kuendesha
masuala ya mazingira. Mkazo wa kuhifadhi na kusimamia mazingira ni
kwa ajili ya kukuza uwezo na akili za jamii na watu binafsi katika kudumisha
usimamizi kwa manufaa yao na manufaa ya vizazi vijavyo. Inatia moyo kwamba
juhudi hizo zimeamsha fahamu za watu, moyo wa kupenda na vitendo vya kusaidia kwa sababu zaidi ya
idadi 159 ya CBO’s (Community Based Organiations) na NGO’S (Non-Governmental
Organisations) zimeundwa zikiwemo pia na sekta binafsi na watu binafsi kujiunga
katika mkumbo. Isitoshe, Serikali kwa
kushirikiana na mashirika na mawakala kama vile CBO’s/NGO’s wanatekeleza mipango
mbalimbali katika maeneo ya mijini na vijijini.
Vyombo vya habari (radio, televisheni, magazeti) vimefanyaka kazi nzuri
katika kuhamasisha na kutangaza vipindi
mbalimbali vya elimu kuhusu masuala ya mazingira na hivyo kutoa mafunzo kwa
hadhara na watu binafsi ya kuwa na moyo wa kupenda, kujituma na kufahamu jinsi
ya kuhifadhi na kusimamia mazingira.
Serikali ilitumia sera za
sekta zinazohusiana na misitu, madini, wanyama pori, samaki, kilimo, mifugo na
ardhi ambazo zimeweka kipaumbele masuala ya usimamizi na hifadhi za rasilimali
na mazingira, kukuza kufahamu wa wananchi wa kuelewa uhusiano kati ya mazingira
na uhai na kuendeleza ushirikiano wa kimataifa kuhusu ajenda ya mazingira.
Ni dhahiri kwamba uhifadhi
na usimamizi wa mazingira duniani na kitaifa una nia ya kushinda matatizo
yanayotokana na umaskini, maradhi, hali mbaya na duni ya upatikanaji wa
chakula, makazi machafu, maji yasiyo salama, upatikananji wa nishati
usioridhisha na ukosefu wa ajira.
Kuelewa kwa wananchi na
watu binafsi juu ya faida za kuhifadhi na kusimamia mazingira ndiyo msingi wa
kuendeleza rasilimali na mazingira. Hiyo
inakwenda sambamba na utekelezaji wa mipango thabiti ya kuondoa umaskini kwa
sababu umaskini unaendana na matumizi mabaya ya rasilimali na uharibifu wa
mazingira na hivyo juhudi za kuuondoa umaskini zinahitaji ushirikiano wa jinsia
zote. Zaidi ya hayo, serikali imeamua
kushughulikia hifadhi na usimamizi wa mazingira pamoja na kuondoa umaskini
ukishirikiana kikamilifu na watu binafsi, CBO’s, NGO’s na wafadhili.