Wateja kupokea muda wa maongezi wa shilingi 50 bure kila watumapo fedha kwa watuamijiwa M-Pesa waliojiandikisha.
Kampuni ya simu ya Vodacom leo (June 26) imezindua ofa
ambayo itawafanya wateja wote wa M-pesa waliojiandikisha kupata muda wa
maongezi kwa kila watumapo ama kupokea fedha.
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Rene Meza ametangaza kutolewa
kwa muda wa maongezi wa ziada wa shilingi 50 kwa wateja watakaotuma ama kupokea
fedha kwa njia hiyo na kuongeza kuwa wateja wataweza kuutumia muda huo kupiga
simu Vodacom kwenda Vodacom na kutuma ujumbe mfupi wa simu kwenda mtandao
wowote nchini.
“Jinsi mtu anavyotuma
ama kupokea zaidi fedha kwa M-pesa, ndivyo atakapata zaidi muda wa maongezi wa
ziada, alisema.
Meza amesema promotion hiyo ina lengo ka kuwatuza wateja wa
Vodacom kwa kuendelea kuwa watumiaji wazuri wa mtandao huo.
“Promotion hii inaifurahisha Vodacom kwakuwa itawahimiza
wateja wetu zaidi kutumia M-pesa na kuwaruhusu kuona jinsi M-pesa inavyoweza
kubadilisha maisha yao wakati wakifurahia muda wa ziada wa maongezi na kutuma
sms,” alieleza na kuongeza kuwa M-pesa inabakia kuwa miongoni mwa huduma muhimu
zilizoanzishwa na Vodacom nchini Tanzania.
Chanzo: Leotainment blog