GF Trucks & Equipment yawahamasisha wakulima

na Mwandishi wetu   KAMPUNI ya GF Trucks & Equipments, imewataka wakulima na wajasiriamali mijini  na vijijini kuchangamkia pungu... thumbnail 1 summary

na Mwandishi wetu
 
KAMPUNI ya GF Trucks & Equipments, imewataka wakulima na wajasiriamali mijini  na vijijini kuchangamkia punguzo na ofa ya magari ya kubebea maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na magari  ya mizigo kwa ajli ya kuchukulia mazao mashambani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi  wa magari hayo uliofanyika katika viwanja vya maonyesho ya 36 ya biashara ya kimataifa jijin Dar es Salaam, Ofisa Masoko Mwandamizi wa kampuni hiyo, Juma Hamsini, alisema kampuni imeamua kuagiza kwa wingi magari hayo ambayo yatatumika kubebea maji katika ukubwa tofauti kuanzia tani 3 hadi 10.

Aliongeza kuwa wamegundua nchi ina tatizo la nyenzo za kubebea maji pindi kunapotokea tatizo la uhaba wa maji hasa kwa maeneo ya mijini na kwamba hata kwa wakulima wanao uwezo wa kujikusanya na kuunda vikundi ambavyo kwa kupitia benki yoyote nchini wanaweza kudhaminiwa na kukopeshwa magari hayo.

Alisisitiza kuwa kwa upande wa wakulima wanaotegemea umwagiliaji katika sehemu ambazo zina uhaba wa maji pia wanaweza kukodisha kwa kubebea maji na kuuza kama mradi katika eneo husika.

Hamsini alisema kuwa GF wana utaratibu wa kukopesha vitendea kazi kwa wakandarasi, taasisi binafsi na mamlaka za serikali kwa utaratibu maalumu ambapo wana mikopo ya aina mbili moja ni kati ya kampuni na mteja na nyingine ni kati ya kampuni na mashirika ya serikali kama vile halmashauri, manispaa au wizara.

Chanzo: Tanzania Daima