Mussa Mwangoka, Katavi
POLISI
wilayani Mpanda katika mkoa wa Katavi
inawashikilia watu 10 miongoni mwao wakiwemo
wanawake wawili kwa tuhuma ya kukamatwa na nyara
za Serikali zenye thamani ya zaidi ya
Sh milioni 80 kinyume cha Sheria .
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari alisema kuwa
watuhumiwa hao waliokamatwa katika matukio
tofauti wilayani humo kufuatia msako
mkali ulioshirikisha Jeshi la Polisi, askari
wanyamapori kutoka Tanapa na Hifadhi ya Taifa ya
Katavi .
Alidai
kuwa pamoja na kuwakamata watuhumiwa
hao katika msako huo pia timu
hiyo ya askari ilikamata meno ya tembo
matano yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 73
nyama ya nyati yenye thamani ya zaidi ya Sh
milioni 7.2.
Pia
misumeno 5 , mizani miwili , mabegi manne na
magari mawili aina ya Noah yalikamatwa kufuatia
msako huo, ambapo katika tukio la watuhumiwa watano
walikamatwa katika kijiji cha Msaginya wilyani
humo katika Barabara ya Mpanda – Tabora wakiwa na
meno ya tembo matatu yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 50
kinyume cha sheria.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Joseph Mahundi
maarufu kama Ngondo (59), makzi wa Kigoma , Msafiri Nyirawi
(36) na Abubakari Mhina (25) ambaye ni
dereva wote wakiwa wakazi wa mjini Dodoma .
Wengine
ni pamoja na Peter Mashihamvula (55) mkazi wa kitongoji
cha Kawajense mjini Mpanda na David Simwanza
(38) mkazi wa kijiji cha Lwasho wilyani
Mbozi katika mkoa jirani wa Mbeya .
Kwa
mujibu wa Kamanda Kidavashari nyara hizo za
Serikali zilikamatwa zikiwa zinasafirishwa
kuelekea mjini Dodoma katika gari
aina ya Noah yenye namba za usajiri T983
TZJ lililokuwa likiendeshwa na Mhina.
Katika
tukio jingine lililotokea juzi saa kumi
jioni watu watatu wakiwemo wanawake wawili
walikamatwa wakiwa na meno mawili ya tembo yenye
thamani ya zaidi ya Sh milioni 24 kinyume
cha sheria.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Rose Bwigilo (36)
mkazi wa Kimara Mwisho Jijini Dar Es Salaam , Adelina
Alphonce (39) mkazi wa Tabata na John
Venance (26) akiwa pia mkazi wa Jijini Dar Es Salaam.
Siku
hiyo ya tukio kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari watuhumiwa
hao wa likamatwa na nyara hizo katika
gari la aina ya Noah yenye namba za
usajiri T463 BZW iliyokuwa ikiendesha na John pia
msumeno , na mizani vilikamwatwa vikiwa vimefichwa
ndani ya gari hilo.
Katika
tukio jingine watu wawili walifahamika kuwa ni Juma
Ngeleka (30) mkazi wa kitongoji cha Kawajense
mjini Mpanda na John Mlelwa (25) mkazi wa Inyonga
wilyani Mlele wamekamatwa na nyama ya nyati yenye
thamani yenye zaidi ya Sh milioni 7.5.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kidavashari watuhumiwa hao
walikamatwa Juni 28 mwaka huu wilayani humo
ambapo msako bado unaendelea ili kuwabaini
watuhumiwa wengine .
Mwisho