TCU yataja vyuo vikuu vyenye sifa

Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imetoa orodha ua vyuo vya elimu nchini ambavyo inavitambua. TCU pia imewataka wananchi kutembelea tovuti y... thumbnail 1 summary
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imetoa orodha ua vyuo vya elimu nchini ambavyo inavitambua.

TCU pia imewataka wananchi kutembelea tovuti yake ili kutambua vyuo halali vinavyotambulika kwa lengo la kuepuka utapeli.

TCU ilitoa orodha ya vyuo hivyo kupitia katika tangazo lililosainiwa na Katibu wake Mtendaji, Profesa Sifuni Mchome.

Taarifa hiyo ilivitaja vyuo 61 ambavyo vinatambulika na TCU kuwa ni Chuo cha Ardhi, Catholic of Health and Allies Science, Eckernford Tanga University, Hurbert Kiruki Memorial, International Medical and Technological, Katavi University of Agriculture, Mbeya University of Science and Technology.

Vingine ni Mount Meru University, Muhimbili University of Health and Allied Science, Muslim University of Morogoro, Mzumbe University, Nelson Mandela African Institute of Science and Technology, Open University of Tanzania, SebastianKolowa Memorial, Sokoine University of Agriculture, St. Augustine University of Tanzania, St. Johns University of Tanzania, St. Joseph University of Tanzania na Chuo Kikuu cha Zamzibar.

Vingine niTanzania International University, Teofilo Kisanji University, Tumaini University Makumira, United African University of Tanzania, University of Arusha, University of Bagamoyo, University of Dar es Salaam, University of Dodoma, Zanzibar University, Archbishop Mihayo University College of Tabora, Dar es Salaam University College of Education, Iringa University College na Jordan University College.

Vingine ni Josiah Kibira University College, Kampala International University, Kilimanjaro Christian Medical College, Mkwawa University College of Education, Moshi University College of Cooperative and Business Studies, Mwenge University College of Education, Ruaha University College, St. Francis University College of Health and Allied Sciences na St. Joseph University College of Agricultural Sciences and Technology.

Vingine ni St. Joseph University College of Infornation Technology, St. Joseph University College of Management and Commerce, Stefano Moshi Memorial University College, Stella Maris Mtwara University College, Tumaini University Dar es Salaam College, University College of Education Zanzibar, Aga Khan University-Tanzania Institute of Higher Education na Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology-Arusha Centre.

Vingine ni Mzumbe University-Dar es Salaam Centre, Mzumbe University-Mbeya Centre, St Augustine University-Bukoba Centre, St. Augustine University-Msimbazi Centre, St. Augustine University-Songea Centre, St. John  University of Tanzania-Msalato Centre, St. John  University of Tanzania-St. Marks of Dar es Salaam, Stephano Moshi Memorial University College-Mwika Centre, Stephano Moshi Memorial University College-Town Centre, Tumaini University-Mbeya Centre, University of Arusha-Buhare Centre na University of Dar es Salaam-Institute of Marine Science.

Una taarifa, picha za usafiri wa anga, mazingira, maliasili na utalii? tutumie kupitia kingkahindi@gmail.com