Blog ya tabianchi
inalipongeza gazeti la Tanzania Daima kwa kuweka kipaumbele na
kuchapisha habari za mazingira, maliasili na utalii. ujasiri huu wa
kutoa nafasi kwa habari za aina hii umekuwa ukifanywa na vyombo vya
habari vichache sana na pale chombo fulani kinapoonyesha jitihada hizo
mimi kama mdau wa masuala ya mazingira, maliasili na utalii na Mtanzania
yeyote yule mwenye mapenzi ya kweli na nchi yake hatuna budi kutoa
shukran na pongezi zetu.
Nimekuwa
nikifuatilia mara kwa mara magazeti yetu hapa nchini kwa zaidi ya miezi
miwili sasa na nimebaini kuwa habari za aina hii hazipewi nafasi
ipasavyo pamoja na kwamba zinagusa maslahi ya jamii.
Kama
ilivyokauli mbiu ya tabianchi, vita ya mabadiliko ya tabianchi ni ya
kila mmoja, hivyo napongeza na kuhamasisha jamii yote kushiriki katika
vita hii ikiwa ni pamoja na kutunza, kuhifadhi, kutangaza na kutembelea
hifadhi zetu za taifa na makumbusho ya taifa.
Habari na makala haya hapa chini yote yamechapishwa leo katika gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, 11, 2012
Nyalandu awabomoa TANAPA
Bahi wakataa urani kuchimbwa
Watakaoharibu mazingira Muheza kuchapwa viboko
Watalii kukosa walichokitarajia ni kuporomosha uchumi
Mkuhumi na mkakati wa kupunguza umaskini kwa wananchi
REDD + iungwe mkono kuhifadhi sekta ya misitu, kukuza uchumi wa kijani
Una taarifa, picha za usafiri wa anga, mazingira, maliasili na utalii? tutumie kupitia kingkahindi@gmail.com