ZIPO nchi kadhaa duniani zilizoendelea na kuneemeka kwa kutegemea
utalii katika kukuza uchumi wake, ambazo zimekuwa zikisimamia vyema
kuulinda na kuukuza, kwa lengo la kuwafanya watalii wa ndani na nje
kuongezeka kila siku.
Tanzania ni moja ya nchi chache duniani ambazo zingeweza kuongeza kasi
ya kukuza uchumi wake kutokana na kuwa na vivutio vingi vya utalii,
zikiwemo mbuga kubwa na nzuri za wanyama, Mlima Kilimanjaro, mito na
mabonde yanayowavutia watalii hususan wa nje kuja kutembelea kwa kulipa
fedha za kigeni.
Leo unapozungumzia pato linalochangiwa na sekta ya utalii, utakuwa
unazungumzia jambo ambalo halina uhakika kwa kuwa utalii unazidi
kuporomoka kila kukicha kutokana na sababu mbalimbali, ambazo pia
zinawafanya watalii wengi kusitisha safari zao kutoka makwao kwa gharama
kubwa kuja Tanzania.
Utalii ni sekta inayotumika kuingiza fedha nyingi za kigeni, lakini
iwe kwa kuwashawishi wageni kuingia kwa wingi na wakutane na kile
wanachokitarajia na wakirejea makwao wakasimulie walichokiona ili
waliowasimulia wapate hamu ya kuja kutalii.
Hakika utalii wa Tanzania ulijitangaza wenyewe, haukutangazwa kama
tunavyoona nchi nyingine zikihangaika kuutangaza utalii wake, ili
kuwashawishi watalii kuingia, lakini bila mafanikio.
Leo utalii wa Tanzania umegubikwa na dosari mbalimbali zinazowafanya
watalii wasiridhike kwa kiwango kikubwa, kwa maana ya kutokidhi
matarajio yao, hasa kwa mtalii ambaye alikuja miaka15 iliyopita, hakika
akija leo hatafurahi kwa vile utalii wetu umeporomoka sana.
Soma zaidi
Una taarifa, picha za usafiri wa anga, mazingira, maliasili na utalii? tutumie kupitia kingkahindi@gmail.com