MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII DUNIANI YAFUNGULIWA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo ameipongeza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kufungua ofisi jijini Mwanza kwa kuwa hatua hiy... thumbnail 1 summary

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo ameipongeza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kufungua ofisi jijini Mwanza kwa kuwa hatua hiyo itaharakisha maendeleo ya sekta ya utalii mkoani Mwanza na Kanda ya ziwa na amewataka wananchi wa Mwanza kukuza utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Mwanza, Kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla na kuondokana na dhana kuwa utalii ni kwa ajili ya wazungu tu.


MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII DUNIANI YAFUNGULIWA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo (Mwenye suti nyeusi) akikata utepe kuashiria
ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Utalii duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani Mwanza.


Eng. Evarist Ndikilo amayasema hayo wakati akizindua maadhimi misho ya siku ya Utalii duniani ambayo kitaifa mwaka huu yanafanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa Nyamaga. Amesema mkoa wa Mwanza una vivutio vingi sana vya utalii ingawa bado havijatangazwa kikamilifu lakini kufunguliwa kwa ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania, kupata fursa ya kuandaa maadhimisho ya siku ya Utalii duniani kwa mara ya pili mfululizo pamoja na ujenzi wa uwanja mpya wa Kimataifa wa ndege wa Mwanza ni masuala ambayo yatachagiza maendeleo ya sekta ya Utalii mkoani Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla.


MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII DUNIANI YAFUNGULIWA

Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania –TTB Bw. Geofrey Tengeneza
akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo
namna Bodi hiyo ya Utalii inavyotekeleza majukumu yake.


Pamoja na hayo mkuu huyo wa mkoa ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana kwa karibu sana na Chama cha Utalii Mkoani Mwanza (MTA) na akasisitiza umuhimu wa kuwashirikisha waandishi wa habari wa mkoani Mwanza katika kusaidia kutangaza vivutio vya mkoa huu na kanda nzima ya Mwanza “ Niiombe Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana kwa karibu na MTA na wadau mbali mbali wa sekta ya utalii mkoani Mwanza bila kusahau kuwashirikisha wandishi wa habari kwani kalamu zao zitatusaidia sana katika kutangaza vivutio vyetu vya Mwanza na kanda ya ziwa” alisema Eng. Ndikilo


MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII DUNIANI YAFUNGULIWA

Eng. Evarist Ndikilo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza akitia saini kitabu cha wageni katika
banda laWizara ya Maliasili na utalii wakati akitembelea mabanda ya maonesho katika
uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza muda mfupi baada ya kufungua maadhimisho ya
siku ya utaliiduniani yanayofanyika Kitaifa mkoani Mwanza. Kulia kabisa ni Mkurugenzi
msaidizi wa Idara ya Utalii Bibi Uzeeli Kiangi.


Akizungumzia kauli mbiu ya maadhimisho hayo isemayo “Utalii na Maji kulinda hatma yetu” Mkuu huyo mkoa amesema ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda vyazo vya maji na kuhakikisha kuna kuwa na matumizi sahihi na endelevu ya maji kwani maji ni muhimu sana kwa maendeleo ya sekta ya utalii. Amedokeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za shirika la Utalii duniani UNWTO matumizi ya maji duniani yanatarajiwa kuongezeka maradufu kutokana na kuendelea kuongeza kwa watalii duniani na miundo mbinu mbalimbali ya sekta ya utalii duniani.

Mapema mkuu huyo wa mkoa ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi aitembelea mabanda ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji, taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na binafsi na wadau wa sekta ya utalii wanaoshiriki maonesho hayo kutoka Dar es salaam, Mwanza, Kagera, na nchi jirani ya Uganda.

Maadhimisho hayo yatafikia kilele chake Septemba 27, 2013 ambayo ndiyo siku ya Utalii duniani, lakini yatahitimishwa tarehe Sptemba 29, 2013.

Chanzo: TTB