Wito unatolewa kwa wananchi hususan wanaoishi
karibu na Hifadhi za Taifa,Mapori ya Akiba na Maeneo Tengefu kusaidiana
na wahifadhi katika kulinda,kutunza na kuhifadhi wanyama wetu kwa kutoa
taarifa mara kwa mara wanapoona watu wanaohujumu maliasili zetu.Uporaji
wa meno ya Tembo na biashara haramu ya wanyamapori na mzao yake,pamoja
na uvamizi wa mifugo katika maeneo yaliyohifadhiwa ni jambo linaloumiza
vichwa vya wazalendo wa nchi yetu.
Kukosekana kwa uzalendo wa baadhi ya Watanzania kunaweza kukapelekea kumalizika kwa mazao yanayotokana na wanyama mbali mbali hususan Tembo na hivyo kupotea kwa spish hizo na kubakia na historia kwamba hapo zamani za kale ilikuwa Eden ya wanyamapori wazuri,wakubwa na wa kila aina.
Pichani ni moja ya mitego ya waya iliyotegwa na majangili iliweza kumnasa simba lakini simba huyo ailifanikiwa kuing'oa na kuondoka nayo lakini mdhala aliyopatikana nayo yalikua makubwa sana.

TUSHIRIKIANE KUWALINDA WANYAMA NA KUYALINDA MAZINGIRA.